Kiwanja cha Ndege cha London kutotumia mtu yeyote katika eneo la kuongozea ndege uwanjani! #Teknolojia

0
Sambaza

Fikiria kiwanja cha ndege kilichokuwa na safari nyingi sana kila muda ndege zinapaa na kutua – alafu sehemu ya kuongozea ndege na kutoa msaada wa kutua na kuondoka uwanjani hapo KUTOKUWA na mtu yeyote kabisa katika eneo hilo.

Basi ndio teknolojia inayokuja kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha London cha nchini Uingereza.

Kiwanja cha ndege hicho kinakuwa moja ya viwanja vichache duniani kote kuanza kutumia teknolojia kubwa ya kidigitali kuhakikisha huduma inaboreshwa kwa kutumia teknolojia za kisasa hasa hasa kwenye masuala ya hali ya hewa na kamera za kisasa ili kumsaidia muongozaji ndege katika kiwanja cha ndege kuweza kujionea mengi zaidi na kwa urahisi zaidi.

Kiwanja cha Ndege cha London

Kiwanda cha ndege cha jiji la London ni moja ya kiwanja muhimu hasa hasa kwa wafanyabiashara kwa kuwa kipo karibu na maeneo muhimu ya kibiashara ya jiji la London

eneo la kuongozea ndege

Kwa kawaida huu ndio muonekano wa eneo la kuongozea ndege, ambalo ndani yake kuna kuwa na kundi la watu wanaosaidia kutoa muongozo kwa marubani wanaoendesha ndege. Eneo hilo kwa sasa litachukuliwa na mifumo ya kamera mbalimbali za ubora wa HD.

Nini kipya?

Eneo la mnara wa kuongozea ndege hakutakuwa na watu ndani yake bali kutakuwa na kamera 14 zinazochukua picha (video) za moja kwa moja katika ubora wa HD. Pia kutakuwa na sensa mbalimbali za kuweza kugundua mabadiliko mbalimbali ya vitu eneo la uwanja. Kamera hizo zitaweza kuchukua picha za moja kwa moja za HD katika eneo la uwanja wa ndege.

  • Video hizo za moja kwa moja, yaani mubashara zitakuwa zimeunganisha moja kwa moja kupitia nyaya za intaneti ya kisasa na haraka (fiber) na kutuma taarifa hizo moja kwa moja kwenye kijiji kingine kilicho umbali wa takribani kilometa 110 kutoka kiwanja hicho cha ndege.
  • Katika ofisi ya kijiji hicho kutakuwa na vioo/display kubwa za kuonesha taarifa zote zinazopokelewa muda huo hii ikiwa ni pamoja na hali ya hewa na muonekano mzima wa eneo la kiwanja cha ndege.
SOMA PIA:  Facebook kujiweka pembeni na vitu vyenye maudhui ya kutia shaka

Muongozaji ndege ataweza kuona mambo mengi kwa haraka na urahisi zaidi ukilinganisha na kama angekuwa kwenye chumba cha mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege.

Je ni salama dhidi ya udukuzi?

Kwa kiasi kikubwa itakuwa hatari sana kama mawasiliano ya kutoka kwenye kamera zilizokwenye uwanja kudukuliwa kwani kunaweza sababisha ajali. Kampuni iliyotengeneza teknolojia hiyo imehakikisha mfumo mzima unakuwa unajitegemea na upo salama, na pia waya za fiber za mawasiliano katika ya kiwanja cha ndege na ofisi iliyo umbali wa zaidi ya kilomita 100 zitakuwa tatu. Moja itakuwa ndiyo kuu na itakuwa inatumika na nyaya zingine mbili zitakuwa za ‘backup’ ili kusaidia kama hitilafu itatokea kwenye waya wa mawasiliano wa kwanza.

SOMA PIA:  Kusitishwa kwa utumikaji wa Windows Vista

Teknolojia hiyo imetengenezwa na kampuni ya Saab Digital Air Traffic Solutions ya nchini Sweden na imefanyiwa majaribio ya kiusalama na ubora kwa miaka 10.

Ajira je?

Uongozi wa shirika la huduma za ndege nchini humo umesema hakuna atakayepoteza kazi katika kitengo hicho. Wafanyakazi wote watapatiwa mafunzo zaidi ya jinsi ya kutumia teknolojia hiyo mpya.

Teknolojia hii kwa sasa inatumika kwenye viwanja vingine vya ndege viwili tuu nchini Swideni na tayari vipo viwanja vya ndege vinavyotaka kutumia teknolojia hiyo.

Pia kiwanja cha ndege cha London ndio kinakuwa kiwanja kilicho na wastani wa safari nyingi zaidi za ndege kuanza kutumia teknolojia hii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com