Kodi kupanda kwa wamiliki wa tovuti za habari Tanzania - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kodi kupanda kwa wamiliki wa tovuti za habari Tanzania

0
Sambaza

Tovuti za habari nchini Tanzania na ulimwenguni kote zimekuwa chanzo cha habari katika ulimwengu wa teknolojia na kufakia watu kiurahisi zaidi kupitia vifaa mbalimbali vya kidijitali.

Katika ulimwengu wa teknolojia blog/tovuti ina sehemu kubwa katika kuwafikia wale ambao unawalenga kitu hucho kifike kwao lakini ulishawahi kujiuliza kinachofanyika ili kuifanya tovuti (blog) kuwa hewani?

Gharama kadha wa kadha huwa zinalipwa na mojawapo ni leseni ya biashara, jina la tovuti, upatikanaji wake kwenye intaneti, n.k. Katika siku za hivi karibuni imeelezwa kuwa go to link sasa wamiliki wote wa blog itabidi walipe kiasi cha pesa zitakazoingia serikalini.

Ili kuidhinisha kama mtoa habari kwa njia ya mtandao mwombaji ibidi ajaze fomu kuweka http://noroozipc.com/contact/ makadirio ya kiasi cha fedha alichowekeza, idadi ya wakurugezi, wanahisa, kiasi cha hisa wanazomiliki, viwango vya elimu vya wafanyakazi wao, tarehe wanayotarajia kuanza kazi na bila kusahau mpango mkakati wa ukuaji wa biashara yao.

tovuti za habari

Tovuti za habari nyingi zimekuwa na muonekano mzuri na hata kuweza kuwa na mwonekano wa kuvutia mtu akitembelea tovuti husika kupitia simu janja, tabiti, n.k.

Kwanza mamlaka husika itahakiki watoa habari wote kwa njia ya tovuti (bloggers) kisha kutakiwa kulipa kiasi cha $930|Tsh. 2,092,500 kwa mwaka ili kutambulika na kupewa leseni.

Hata baada ya blog kuidhinisha kufanya kazi zake bado mamlaka husika itakuwa na nguvu ya kuamuru makala fulani iondolewe kama inaonekana inaleta click uchochezi, kuhatarisha usalama wa nchi, inachukiza na kuamuru makala husika kuondolewa ndani ya saa 12 vinginevyo kulipa faini ya $2,210 au kwenda jela mwaka mmoja.

Hata wale wanaotoa matangazo ya redio, televisheni kwa njia ya intaneti nao tozo ya $930 kila mwaka itawahusu na huenda ikaathiri upatikanaji wa habari.

tovuti za habari

Uwezo wa tovuti kufikia watu wengi kwenye mitandao ya kijamii imesaidia watu kupata habari kutoka kwenye tovuti makni inayosimamia weledi na miiko ya kazi zake.

Kama unfikiria kuanzisha blog yako basi haya ni machache tu ambayo inabidi uanze kuyafikiria namna ambayo utayaweka sawa na kila kitu chako kuhusu utoaji wa habari kwa njia ya mtandao kiende sawa.

Vyanzo: Quartz Africa, iAfrikan

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.