Kompyuta milioni 600 zinatumia toleo la Windows 10

0
Sambaza

Ingawa Microsoft walianza na lengo kubwa la kufikisha vifaa bilioni 1 vinatumia toleo la Windows 10 kufikia mwaka 2018, baada ya kulisoma soko vizuri walibadika. Kufikia Novemba toleo la Windows 10 linatumika katika vifaa milioni 600.

Lengo la kufikisha watumiaji bilioni 1 kufikia mwaka 2018 ungefanikiwa tuu kama kampuni ya Microsoft ingeendelea kutoa toleo la Windows 10 bure kwa watumiaji wote wa matoleo ya nyuma ya Windows, mfano: Windows 7 na Windows 8.

SOMA PIA:  Jinsi gani unaweza kuigawanya diski uhifadhi #Maujanja

Kushindwa kwa Microsoft katika biashara ya simu janja kutachangia kwa kiasi kikubwa kutokanikiwa kwa kasi kwa watumiaji na vifaa vingi zaidi kuwa na toleo la kisasa la Windows 10.

airtel tanzania bando

Mwanzo wa mwaka huu Microsoft walisema toleo la Windows 10 lilifanikiwa kuwekwa katika vifaa milioni 500 na data zinaonesha wingi wa kuwekwa kwenye vifaa vipya umezidi kushuka tokea toleo hilo liache kutolewa bure.

Statcounter:

Kompyuta milioni 600 zinatumia toleo la Windows 10

Data za tovuti ya StatCounter: Inaonekana toleo la Windows 10 linazidi kutumika zaidi

Data za tovuti ya netmarketshare.com bado zinaonesha Windows 7 ndilo toleo linalotumika zaidi lakini bado utumiaji wa Windows 10 unazidi kukua

Microsoft: Kompyuta milioni 600 zinatumia toleo la Windows 10

Ila bado kufikisha idadi ya kutumika kwenye vifaa milioni 600 ni mafanikio makubwa kwa Microsoft. Data mbalimbali zinaonesha toleo la Windows 10 tayari ndilo linalokua zaidi katika utumiaji kuliko matoleo mengine ya programu endeshaji katika kompyuta.

SOMA PIA:  Hii ndio kampuni inayoongoza kwa mauzo ya Kompyuta duniani (Robo ya pili, 2017)

Vipi kwako unatumiaji toleo gani la Windows? Je unaamini Windows 10 ni bora zaidi?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com