Facebook inaendelea najitihada zake za kuwafanya watumiaji kutumia muda mwingi zaidi katika mtandao huu ulioanzishwa mwaka 2004, Facebook imeleta uwezo wa watumiaji wake kuagiza chakula mtandaoni bila ya kutoka katika mtandao.
Watumiaji wataweza kuagiza chakula kutoka katika migahawa iliyoorodheshwa na kuletewa/kuchukua chakula chao bila ya kuhitaji kutembelea mitandao ama kurasa za migahawa hiyo.
Hii inamaana kwamba Facebook wakishirikiana na migahawa iliyoorodheswa watawezesha migahawa hiyo kupokea oda za chakula na kukifikisha kwa wateja wao.
Facebook wanafanya hivi kwasababu wanataka ikiwezekana tufanye kila kitu ndani ya mtandao huu, wanataka tutumie mtandao huu kwa kila kitu tunachofanya katika mitandao ya jamii.
Kimsingi kama tutafanya mambo mengi katika mtandao huu maana yake ni kwamba Facebook ataingiza pesa zaidi katika matangazo ndio maana tumeona mtandao huu ukijaribu kuleta huduma tofauti tofauti.