Utaweza Kubackup Kompyuta Nzima kupitia Google Drive

0
Sambaza

Google wanaleta maboresho mapya katika app/programu yao maarufu ya Google Drive. Kupitia Google Drive utaweza kubackup kompyuta nzima.

Programu ya Google Drive kwenye kompyuta kwa kipindi kirefu iliwezesha mtumiaji kuweza kuwa na nakala ya mafaili yake salama kabisa mtandaoni kama tuu yamewekwa kwenye folda la Google Drive.

Kuanzia mwisho wa mwezi huu kutakuwa na sasisho jipya la Google Drive litakalomwezesha mtumiaji kuchagua ata mafolda mengine mengi ata ‘Desktop’.

kubackup kompyuta nzima google drive

Muonekano wa programu hiyo, hapa ikiwa inatumika kwenye kompyuta ya Macbook

Uwezo huo utakapokuja app haitaitwa Google Drive tena bali itatambulika kwa jina la Backup and Sync app na itakuwa mjumuhisho wa app za Google Drive na Google Photos – yaani itaondoa ulazima wa zamani ambapo mtumiaji ilibidi awe na programu mbili.

SOMA PIA:  Facebook: WhatsApp yafikisha watumiaji bilioni 1.5 kwa mwezi

Changamoto kubwa kwa watumiaji wengi itakuwa ni kiasi chao cha uhifadhi wa Google Drive mtandaoni tuu. Kwani kwa sasa Google inawapa watumiaji wote GB 15 bure za mafaili, na ujazo wa bure (unlimited) kwa uhifadhi wa picha. GB 100 ya Google Drive kwa mwezi ni takribani Tsh 4,000, wakati TB 1 ni takribani Tsh 20,000 kwa mwezi. 

App ya hii mpya itaanza kupatikana kwa watumiaji wa Windows na Macbook tarehe 28 mwezi Juni.

SOMA PIA:  Simu janja mpya kutoka kwa Google zina matatizo ya kiufundi

Je huwa unatumia programu hizi spesheli za kubackup mafaili salama mitandaoni? Je boresho hili la huduma ya Google Drive kutoka Google unalionaje?

Chanzo: PCMag na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com