Namna ya kubadili folda lako kuwa la rangi uitakayo katika Windows! #Maujanja

0
Sambaza

Tofauti na mfumo endeshi wa Mac OS X, mfumo endeshi wa Windows haurusuhu kubadili rangi kwa mafolda yake.

Hii ina maana kwamba unaweza kutafuta mafolda kwa kutofautisha majina na si rangi. Kuna programu nyingi za kompyuta zinazoweza kukufanyika kazi hiyo ya kubadili rangi ya mafolda yako na kuyafanya kuwa yenye kuvutia zaidi.

Leo Teknokona itakusaidia na kukufahamisha kwa wale ambao hawakujua kabla namna ya kubadili rangi mafolda yako katika kompyuta na kuifanya kuwa na muonekano mzuri na nadhifu.

SOMA PIA:  Ifanye kompyuta yako ukiiwasha ikuite jina lako. #Maujanja #Windows

Programu itakayo kusaidida kubadili rangi za mafolda yako ni Folderico. Programu hii inapatikana bure na ni ndogo sana yenye takribani MB 4.

Hatua za kufuata kubadili rangi ya Folda lako;

1. Kwanza kabisa pakua programu ya Folderico.

Imefanyiwa majaribio na haina virus nakuwekea Link yake ili uipakue
Bonyeza hapa ili uipakue Folderico

2. Baada ya kulipakua, li unzip na fungua folda lenye jina la folderico.exe kwa ajili ya hatua za kubadili rangi ya folda lako katika kompyuta.

Baada ya hapo ngoja nikuwekee picha zitakazokuongoza kufanikisha zoezi lako

folda lako kuwa la rangi uitakayo katika Windows

Anza ku Unzip file lako

Fungua file lililoandikwa folderico.exe

Bonyeza palipoandikwa Select Folder

Anza palipowekwa namba moja na ufuate mpangilio ulivyo

Sasa bonyeza Select icon

Bonyeza palipowekwa mshale kuchagua rangi

Chagua rangi uitakayo sasa

Namna ya kuchagua ni kubonyeza folder lenye rangi uipendayo

Baada ya kuchagua bonyeza Apply kukamilisha zoezi lako

Baada ya kumaliza hatua hizo zote fanya kurefresh kwa kubonyeza right click (F5). Furahia muonekano wa rangi tofauti tofauti kwa mafolda yako.

Usisite kutupa maoni yako kuhusu maujanja haya, kama yamekusaidi anakukuongezea ufahamu wako katika mambo ya Teknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com