Kuchati Facebook Kwenye Simu au Tableti Kutaitaji Messenger

0
Sambaza

Unataka ku’chat’ na rafiki yako kupitia Facebook kwenye simu yako? Itakubidi ushushe programu ya Facebook Messenger.

Facebook wanategemea kuondoa uwezo wa kutumiana meseji ndani ya app ya Facebook kwa simu/tableti ulimwenguni kote ndani ya siku chache zijazo. Katika taarifa yao wiki hii Facebook wamesema tayari wameshaanza maandalizi ya kuondoa uwezo wa kutumiana meseji katika Facebook App na mabadiliko haya yataanza kujitokeza taratibu kwa watumiaji wote duniani kote.

Uamuzi huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na kampuni hiyo katika kutengeneza na kumiliki programu moja moja zilizobora zaidi.

SOMA PIA:  TECNO Kwa Kushirikiana Na Klabu Ya Man City, Wanakuja Na Simu Janja!

Katika kutekeleza mabadiliko haya watumiaji wa programu ya Facebook wakienda sehemu ya kutuma ujumbe watapelekwa moja kwa moja kwenye programu ya Messenger kama wanayo tayari kwenye simu na kama bado hawana watapewa chaguo la kuweza kushusha programu hiyo kwenye simu zao.

Watumiaji wa Moja kwa Moja wa Facebook Kupitia Mtandao Ndio Hawataathirika na Mabadiliko Haya

Watumiaji wa Moja kwa Moja wa Facebook Kupitia Mtandao Ndio Hawataathirika na Mabadiliko Haya

Facebook wanasema kuna takribani watumiaji milioni 200 wa programu ya Messenger duniani, na kuna watumiaji zaidi ya bilione 1.1 wanaotumia Facebook zaidi ya mara moja kila mwezi. Facebook wanadai ya kwamba programu ya Messenger inafanya kazi kwa ubora wa zaidi ya asilimia 20 kwenye kuchati ikilinganishwa na kuchati kwenye programu ya Faceboook. Mambo yanayopatikana katika programu hiyo ni pamoja na uwezo wa kuchati kimakundi (group chat), uwezo wa kutumiana picha na video, na kwenye baadhi ya nchi uwezo wa watumiaji kupigiana simu bure(voice calls), na uwezo wa kutumiana ujumbe wa sauti kama vile kwenye WhatsApp.

SOMA PIA:  Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE

Messenger inapatikana kwa ajili ya Android, iPhone, iPad, pamoja na simu za Windows.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com