Kuharibika kwa Setilaiti ya Facebook, Tanzania na Afrika zimekosa Fursa?

0
Sambaza

Elon Musk na Mark Zuckerberg wana vitu kadhaa wanavyofanana zaidi ya kuwa mabilionea. Wote wana shauku ya kuhakikisha kuwa anga inakuwa ndicho chanzo kikuu cha usambazaji na utoaji wa huduma za intaneti katika miaka kadhaa ijayo.

Mark Zuckerberg Setilaiti ya Facebook

Mwanzilishi wa kampuni ya Facebook

Ingawa kujenga uwezo wa kutumia intaneti ya anga sio jambo jipya, kinachopelekea hasa hawa jamaa kung’ang’ania jambo hili ni uwepo teknolojia mpya na unafuu wa gharama za kurusha vyombo vitakavyotoa intaneti kutoka angani.

Tarehe 1 Septemba, Amos 6 ambayo ni Setilaiti ya Facebook ililipuka wakati ilipokuwa katika kifaa cha kurusha kwenda angani. Kifaa hicho kinachojulikana kama roketi la SpaceX kinatengenezwa na kampuni inayomilikiwa na Elon Musk, bilionea ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini anayeishi Marekani mwenye uraia wa nchi tatu, Afrika Kusini, Canada na Marekani.

SOMA PIA:  Kukosea namba ya mtu anayempigia kwamuwezesha msichana kupata mume

Kusudio kubwa la kurusha setilaiti ya Facebook lilikuwa ni kutoa huduma ya Intaneti kwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika na ilikuwa ni kati ya mipango ya Zuckerberg ya kuiunganisha dunia nzima na intaneti.

Mwanzilishi na mmiliki wa maka,puni ya SpaceX, Solar City na Tesla

Elon Musk, mwanzilishi na mmiliki wa makampuni ya SpaceX, Solar City na Tesla

Kwa Zuckerberg, ambaye kwa miaka kadhaa umekuwa ni mpango wake binafsi kuunganisha dunia kwa intaneti, kuharibika kwa setilaiti hiyo haikuwa habari njema hata kidogo. Katika wakati ambao amekuwa Barani Afrika, eneo Kusini mwa jangwa la Sahara kwa mara ya kwanza akizungumza na wataalamu wa teknolojia na viongozi wa serikali kuhusu mpango wake huu, lazima angesikitika vilivyo.

SOMA PIA:  Marekani kuzidisha katazo la Laptop katika ndege za kimataifa

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Mark aliandika “Wakati huu ambao nipo Afrika, nasikitika sana kusikia kuwa ilishindikana kurusha SpaceX na jaribio hilo liliteketeza kabisa setilaiti yetu ambayo ingetoa intaneti kwa wajasiriamali wengi na kila mmoja katika bara hili.”

Kwa bahati nzuri, Facebook hawajakata tamaa na hivi karibuni watarusha kifaa kingine cha intaneti angani kwaajili ya Afrika. Mark anasema “kwa bahati nzuri tumeendeleza teknolojia nyingine kama vile Aquilla (Drone la Intaneti la Facebook) ambayo itawaunganisha watu pia, bado tutaendelea na mkakati wetu wa kumuunganisha kila mmoja na tutaendelea kufanya kazi hadi siku ambayo kila mmoja atanufaika na fursa zitakazoletwa na Intaneti hii.

SOMA PIA:  Twitter yasema Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa Marekani

Je unadhani mpango huu utafanikiwa? Endelea kuwa nasi kwa muendelezo wa habari hii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com