Jinsi Ya Kuhifadhi Mafaili Katika Mtandao!

Jinsi Ya Kuhifadhi Mafaili Yaliyoko Kwenye Simu/Kompyuta Katika Mtandao!

0
Sambaza

Uzuri wa Teknolojia ni kwamba kama uko makini basi hutaweza kupoteza taarifa zako zozote ambazo zipo katika vifaa vyako kama vile simu na kompyuta…

online Seroquel order

Taarifa hizo zinaweza zikawa katika mfumo wa picha, video, sauti na kadhalika. Labda nikuulize kama ushawahi sikia neno ‘Back Up’?

buy flagyl online ‘Back Up’ ni neno la kimombo ambalo kwa Kiswahili linamaanisha kuhifadhi taarifa kwa kutengeneza nakala ya pili. Nakala hiyo inatumika endapo pale utakuwa umepoteza taarifa za kwanza.

http://kepto.org/fundraisers/shoparoo/ Yaani kama simu nimepoteza picha zangu katika simu yangu (mfano simu iliyoibwa) kama nilihifadhi ‘back up’ katika mtandao basi bila shaka nikipata simu mpya naweza nikarejesha taarifa zangu kama kawaida

Kumbuka ‘Back up’ sio muhimu tuu kama umepoteza taarifa zako, bali unaweza ukawa unatumia kuhifadhi taarifa zako tuu. Kumbuka vifaa vyetu saa zingine huwa vinakuwa vina ujazo mdogo na tunakuwa na mambo mengi sana ya kuhifadhi hapo ndipo umuhimu wa ‘kuhifadhi baadhi ya taarifa’ hizo katika mtandao unakuja

Pengine naongea sana, ngoja nikuonyeshe njia mbili ambazo unaweza ukatumia katika kuhakikisha unahifadhi mafaili yako katika mtandao

INAYOHUSIANA  Mobile Airbag: Kifaa Cha Kuzuia Simu Kupasuka

1. Kwa Kutumia Google Drive

Hapa haijalishi unataka kuhifadhi kitu gani, kuanzia video, sauti, picha n.k vyote utaweza kuvihifadhi humu. Huduma hii ukijiunga nayo kwa mara ya kwanza inakuwa ujazo wa GB 15 za bure ambazo unaweza ukazijaza kwa kuhifadhi mafaili yako. Kwa haraka haraka GB 15 ni sawa na nyimbo 4,000 (kwa makadirio)

Ukihifadhi taarifa (mafaili) yako katika Google Drive basi pale tuu utakapokuwa na kifaa chenye intaneti utaweza kuyapata mafaili yako. Yaani kwa mfano kama simu yako imeisha chaji na mafaili yako yapo katika Google Drive basi unaweza ukayapitia kwa kutumia kompyuta yeyote yenye intaneti.

Uzuri wa Google Drive ni kwamba kila mtu mwenye account ya Google (Gmail) basi anaweza akatumia huduma hii

Google Drive

Google Drive

Unaweza amua kuaangalia vitu vyako humo humo katika Google Drive au ukaamua kuvishusha katika kifaa chako. Kwa mfano kama kuna muziki umeuhifadhi humu una uwezo wa kuucheza humo humo (kama una intaneti) au ukaamua kuushusha katika kifaa chako.

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

Ili kuitumia ingiza taarifa zako za Gmail ambazo ni barua pepe (e-mail) na password (nenosiri).ukishafanikisha hilo basi unaweza ukaanza hifadhi mafaili kwa kubofya katika alama ya +. Unaweza ukapandisha mafaili mengi unavyotaka ili mradi yasizidi kile kiwango cha GB 15. Kama ukiona yanazidi basi unaweza ukaamua kuhamishia mafaili hayo katika kompyuta au katika ‘hard disk’ ya nje

Kwa watumiaji wa iOS wanaweza kuipakua hapa!

Kwa watumiaji wa Android wanaweza kuipakua hapa!

Kwa kutumia kompyuta unaweza ukaipata kwa kuingia >> Drive.Google.com

2. Kwa Kutumia Dropbox

Dropbox haina tofauti kubwa sana na Google Drive. Dropbox yenyewe inatoa ujazo mdogo wa bure wa uhifadhi ambao ni GB 2. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea mtandao wao (www.Dropbox.com) na uingize taarifa zako za muhimu ili kujiunga na huduma hii

Ukishafanikisha hilo basi unaweza ukaanza hifadhi mafaili kwa kubofya katika alama ya +. Unaweza ukapandisha mafaili mengi unavyotaka ili mradi yasizidi kile kiwango cha GB 2.

Dropbox

Dropbox

Kumbuka GB 2 ni ndogo sana, hapa inakubidi uwe na tabia ya kuhamisha vitu mara kwa mara katika kompyuta yako au ‘hard disk’ ili mradi kuhakikisha kuwa ujazo huo haujai. Ila pia Dropbox wanaweza kukuongezea kwa kila unapoalika watu wengine katika huduma hiyo.

INAYOHUSIANA  Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

Kwa watumiaji wa iOS wanaweza kuipakua hapa!

Kwa watumiaji wa Android wanaweza kuipakua hapa!

Kwa kutumia kompyuta unaweza ukaipata kwa kuingia >> https://www.dropbox.com/

Najua wengi tumezoea kuchemeka USB na kuunganisha simu janja na kompyuta zetu ili kupata mafaili tunayotaka kuyahamisha lakini zoezi hili ni rahisi sana kwa kutumia uhifadhi wa mtandaoni. Na pia kama nilivyosema unaweza ukaibiwa hicho kifaa chako na taarifa zote zikapotea tena hasa hasa kama wewe ni mmoja kati ya wale ambao hawahifadhi taarifa zao katika mtandao

Niandikie hapo chini sehemu ya comment, wewe unatumiaga njia gani ili kuhakikisha unapata taarifa zako hata kama kifaa chako kikipotea au kuibwa? Ningependa kusikia kutoka kwako

Tembelea TeknoKona kila siku ili upate maujanja na habari mbalimbali zinazohusu Teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.