Wiki chache zilizopita, washika dau mbalimbali wa sekta ya Afya, pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walifanya uzinduzi wa tovuti maalumu kwa ajili ya taarifa kuhusu afya ya figo, uzinduzi uliofanyika mjini Dar es Salaam.
Tovuti hii ina dhumuni la kutoa elimu ya msingi ya afya ya maini na inatokana na juhudi za kutafsiri kitabu cha Figo, kazi iliyofanyika na Dkt. Gabriel Upunda, mtaalamu wa figo kushirikiana na wengine.
Tovuti ya KidneyEducation.com ni ya kimataifa na inatoa taarifa zihusuzo magonjwa ya figo katika lugha mbalimbali kwa kushirikiana moja kwa moja na wataalumu (madaktari) kutoka maeneo husika.
Taarifa zinazotolewa na tovuti hiyo maalumu zinatazamiwa kupunguza ongezeko la magonjwa ya figo duniani kote na ina watumiaji zaidi ya milioni 100 dunia nzima.
Ukiacha lugha ya kiswahili tovuti hiyo inapatikana pia katika lugha zingine mbalimbali za mataifa na jamii nyingi duniani kote.
Tembelea Elimu ya Figo – KidneyEducation.com/swahili
Chanzo: IPPMedia