Kumbukumbu ya miaka 25 kwa tovuti ya kwanza duniani kuwa hewani (Online)

0
Sambaza

Tarehe 6 mwezi wa nane miaka 25 iliyopita website ya kwanza duniani ilianza kuwa hewani kwa mara ya kwanza.

Tovuti kwanza kwenda hewani yatimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

Tovuti kwanza kwenda hewani yatimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

Tovuti ya kwanza kwenda hewani ilionekana kwa mara ya kwanza Agosti 6 1991 ambayo ilikuwa ikielezea undani wa project ya wakati huo iliyoitwa WWW(Wide World Web) na kueleza jinsi ambavyo mtu anaweza akatengeneza web server yake mwenyewe, kuweza kutengeneza tovuti na kurasa zao wenyewe.

Tovuti hiyo ilijulikana kama http://info.cern.ch/hypertext/WWW/TheProject.html (haipo hewani tena) ambayo pia ilieleza jinsi ambavyo mtu anaweza kutafuta kitu kwenye tovuti.

Kwa tafsiri isiyo rasmi WWW ni kiunganishi kinachowezesha kukupeleka kwenye tovuti husika popote utakapokuwa duniani.

Sir Tim Berners-Le aliyekuja na tovuti ya kwanza duniani

Hapo awali ilikuwa ni lazima kutanguliza ‘WWW’ kabla ya tovuti husika ingawa kwa hivi sasa si lazima kuanza na WWW.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Binti afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza makalio!😯😯😯
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com