Kundi la wadukuzi latishia kufanya Pokémon Go kuwa offline Agosti 1

0
Sambaza

Kundi la wadukuzi latishia kulifanya gemu lenye umaarufu sana kwa sasa la Pokémon Go kuwa offline siku ya kwanza ya mwezi wa nane.

Kundi hilo lijulikanalo kama PoodleCorp kwenye mtandao wa Twitter wamesema watafanya severs za gemu hiyo zisifanye kazi na kutokuwa hewani siku ya tar 1/8 baada ya kufanikiwa kufanya hivyo wikiendi iliyopita.

Pokemon

Kundi hilo lilifanya tukio la kufanana na hilo baada ya kuweza kudukua mtandao wa PlayStation na Xbox Live wakati wa Christmass mwaka 2014.

Tuna mpango wa kuziweka servers za Pokémon Go offline kwa sababu ni gemu ambayo ni maarufu sana kwa na hakuna mtu atakayeweza kutuzuia. Tumechagua Agost 1 ili kuwa na muda wa kutosha wa kujipanga ili kufanikisha.

Servers za Pokémon Go zitakuwa offline kwa zaidi ya saa 20. Mbali na Poodlecorp kuweza kutoa taarifa hiyo pia wamesema wanahusika na udukuzi wa akaunti mbalimbali za watumiaji wa Youtube na servers za  the League of Legends kwa kutumia botnet; kifaa ambacho kina gharama zaidi kuliko mahabara za Niantic (developers wa Pokémon Go).

Gemu ya Pokemon Go

Gemu ya Pokémon Go

Haitokuwa mara ya kwanza kwa kundi la wadukuzi kusema kitu jambo fulani na kushindwa kutekeleza hata hivyo inaaminika kuwa safari hii kitu walichokisema kitafanyika kwahiyo watu wajiandae kukosa kucheza gemu hiyo tarehe waliypsema.

Ni matumani ya wengi kuwa jaribio hilo litashindikana na watu watacheza kama kawaida gemu hiyo. Je, wewe umeshawahi kulicheza gemu hilo? Tuambie wewe kama mdau wa gemu hiyo, tishio hilo limekuathiri kiasi gani? 

Vyanzo: TnW, The Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com