Kurasa za Mark Zuckerberg zadukuliwa, je wewe upo salama? - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kurasa za Mark Zuckerberg zadukuliwa, je wewe upo salama?

2
Sambaza

Kurasa za mitandao za kijamii za mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg zadukuliwa.

Akaunti zake za mtandao wa Twitter, LinkedIn na Pinterest zilidukuliwa na kutekwa kwa muda siku ya Jumapili kabla ya wataalamu wa usalama wa mitandao kumudu kuzidhibiti saa chache baadaye.

Mark akiwa katika moja ya presentations

go Mark akiwa katika moja ya presentations

Kundi la wadukuzi la “Ourmine” limedai kudukua akaunti za Zuckerberg. Kundi hilo lilijigamba kwenye ujumbe waliochapisha kwenye mtandao wa Twitter kuwa ndio waliodukua kurasa hizo na wakamtaka Zuckerberg awatumie ujumbe wa moja kwa moja iwapo alikuwa anataka umiliki wa akaunti hizo.

buy nolvadex “Vipi @finkd tumeingia kwenye akaunti zako za Twitter, Instagram na Pinterest, tuna’test’ kiwango chako cha usalama tuu, tafadhali wasiliana nasi”.

zuckerberg zadukuliwa

buy propecia finasteride Ukurasa wa Twitter wa Bw. Mark

Ujumbe huo hata hivyo umefutwa kwa sasa. Japo anaimiliki ukurasa huo lakini Zuckerberg hajachapisha ujumbe wowote tangu mwaka wa 2012.

INAYOHUSIANA  Kodi kwenye mitandao ya kijamii yaanza rasmi Uganda

Wandani wa maswala ya usalama wa mitandao ya Intaneti wanadai kuwa huenda udukuzi wa mwaka wa 2012 wa ukurasa wake wa LinkedIn ndio uliochangia tukio hilo la jana. Kosa likiwa ni kutobadili password yake kwa muda mrefu sana, na hivyo password yake ya LinkedIn ndiyo iliyotumika kuingilia kwenye akaunti zake za Twitter, Pininterest na LinkedIn.

Ingawa ana akaunti Twitter si mtumiaji sana. Ingawa wadukuzi hao walidai ya kwamba waliingia hadi kwenye akaunti yake ya Instagram wenyewe Instagram wamepinga na inasemekana ni kweli hawakufanikiwa katika hilo.

Mara zote hakikisha unabadili password zake za mitandao ya kijamii kila baada ya muda flani – miezi 6 – mwaka. Na pia pale tuu ukisikia habari za tovuti kubwa unayotumia kudukuliwa na password za watumiaji kuwekwa wazi basi na wewe hakikish una badili password yako kama unatumia mtandao husika.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|