fbpx

Mpango wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole wazinduliwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mfumo wa majaribio ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole (Biometric) vya watumiaji umezinduliwa rasmi, tarehe 1 Machi, jijini Dar es Salaam.

Zoezi hilo litahusisha kwa sasa mikoa ya mikoa mitano ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar. Mikoa itakayohusika na mpango huo kwa awamu hii kwa Tanzania Bara ni Iringa, Tanga, Singida, Pwani na Dar es salaam.

Mpango wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole wazinduliwa

Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo katika viwanja vya mnazi Mlimani City, Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema utumiaji wa simu za mkononi umekuwa na udanganyifu katika kutoa taarifa za wanaosajili namba zao huku wengine wakitumia
simu kufanya uhalifu.

INAYOHUSIANA  Tanzania yaongeza ulinzi wa teknolojia kwa wanyama pori

Aliongeza Ili kuondokana na changamoto hizo na pamoja na kupata takwimu halisi ya ya watumiaji wa simu za mkononi kwa ajili kuweka mipango ya kuendeleza sekta ya mawasiliano wanalazimika kuanza mfumo huo wa usajili kwa alama za vidole.

Mfumo huo unaanza kwa majaribio kabla ya kuwa endelevu kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuweka udhibiti katika mitandao na udanganyifu katika usajili wa namba za simu kwa watu kutumia vitambulisho visivyo sahihi ama cha mtu mwingine.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.