'Kusave' Maifaili ya WhatsApp kwenye Memori Kadi

‘Kusave’ Maifaili ya WhatsApp kwenye Memori Kadi! Je inawezekana?

0
Sambaza

Tumepata maswali mara kadhaa kuhusu hili. Je ni jambo linalowezekana, na kama linawezekana je nifanyeje? Kwa kifupi jibu ni ‘Ndiyo’ na ‘Hapana’.

Kwa sasa hakuna chaguo la kufanya mafaili yawe yanahifadhiwa kwenye memori kadi (SD Card) pale unapotumiwa. Na sababu iliyowafanya watengenezaji wa WhatsApp wafanye hivyo ni kwamba kwa kuwa mara zote app ya WhatsApp inategemea uhifadhi kutoka kwenye diski kuweza kufanya kazi na kama tunavyojua sifa moja ya memori kadi ni uwezo wa kuichomoa muda wowote tunaotaka. Kutokana na memori kadi kuwa ni kitu kisichotegemewa sana ndio maana WhatsApp imetengenezwa kutegemea kujihifadhi kwenye memori ya simu.

'Low Disk Space' ukiona kitu kama hichi ufahamu ya kwamba uhifadhi wa diski ya simu umekaribia kujaa

http://mkdesignsuite.com/privacy-policy/ Low Disk Space’ ukiona kitu kama hichi ufahamu ya kwamba uhifadhi wa diski ya simu umekaribia kujaa

Kuwepo kwenye memori ya simu kunaipa uhakika wa kufanya kazi bila muingilio wowote. Lakini pia hali hii inamaanisha kama unapokea mafaili sana basi kuna uwezekano wa memori ya simu (diski uhifadhi) kujaa.

INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

Je, ufanye nini?

Cha kwanza kikubwa unachoweza fanya ni kuweka mpangilio (setting) kwenye app yako ya WhatsApp kufanya mafaili unayotumiwa na watu yasijishushe (download) bila ruhusa yako. Kujifunza kufanya hivyo bofya HAPA kujifunza nini cha kufanya.

Njia nyingine ni kuhakikisha unaenda kwenye faili la WhatsApp panapohifadhiwa mafaili na kuhamisha mafaili yako mara kwa mara na kuyaweka kwenye memori kadi.

Utayahamishaje?

http://icareforchildren.org/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://icareforchildren.org/home/ Shusha app ya ES File Explorer au app nyingine yeyote unayotumia kusomea mafaili na diski za simu yako. [Kuifahamu app ya ES File Explorer zaidi – BOFYA ES FILE EXPLORER TeknoKona]whatsapp-e1421682632467

  • Ingia eneo la diski ya simu (memori ya simu), angalia katika ‘folders’ utaona lililoandikwa source WhatsApp
  • Ndani yake utaona kuna lililoandikwa Media. Lichague na kisha chagua ‘Cut’
  • Kisha nenda kwenye SD Card, yaani memori kadi na kisha tengeneza faili jipya, unaweza liita WhatsApp
  • Paste mafaili uliyoya’cut’
INAYOHUSIANA  Facebook yalegeza masharti kuhusu matangazo ya sarafu za kidijitali

Njia hii inaweza pia ikafanyika kwa urahisi kwa kutumia kompyuta, cha kuelewa ni kwamba uhamishe mafaili yote ya picha na video kutoka kwenye folder la WhatsApp kwenye memori ya simu na uyaweke kwenye folder jipya kwenye memori kadi.

Kumbuka mafaili haya uliyoyahamisha hayatasomeka tena kupitia WhatsApp ila yatapatikana kama kawaida kwenye Gallery ya simu yako.

Ila kwa lengo la kupunguza ujazo wa mafaili kwenye diski ya simu yako kufanya hivi itasaidia.

Soma Pia;
App ya Wiki: ES Explorer kwa Kushughulikia Mambo Mengi kwenye Android

Zuia Picha Mbaya Whatsapp

WhatsApp Haifanyi Kazi Au Imekuwa Nzito? Fanya haya!

Kumbuka kusambaza makala hii kwa wengine na endelea kutembelea TeknoKona ! 🙂

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply