Kusitishwa kwa utumikaji wa Windows Vista

0
Sambaza

Inawezekana wapo wachache ambao bado wanatumia programu endeshaji ijulikanayo kama Windows Vista kwenye kompyuta zao; imefahamika kuwa programu hiyo itakuwa haitumiki tena kuanzia hivi karibuni.

Windows Vista amabayo ilianza kutumika kwenye mwaka 2006 mpaka 2009 na baada ya hapo Microsoft waakacha kuweka programu endeshaji ya Windows Vista na kuhamia kwenye Windows 7 ambayo bado inatumiwa na wengi na kuonekana kutokea kupendwa zaidi kutokana na kuwa OS rafiki.

Microsoft wamethibitisha kuwa ifikapo Aprili 12, watasitisisha kabisa matumizi ya Windows Vista kwenye kompyuta.

Nini cha kufanya?

Kwa yeyote yule ambaye bado anatumia Windows Vista kwenye kompyuta yake ni muhimu akafanya maboresho (upgrade) na kuweka Windows 7 au kwenda kabisa kwenye toleo la hivi sasa abalo ni Windows 10.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa kompyuta yako ina umeme wa kutosha wakati kuiboresha kompyuta yako kwa kuhamia programu endeshaji nyimgine.

Ili kuweza ku’upgrade na kwenda kwenye Windows 7 bila kutumia CD unabonyeza kitufe cha Start>>All Programu>>Windows Update kuweza kupata masasisho yatakayokuwezesha kuhama kutoka OS moja na kwenda OS nyingine.

SOMA PIA:  Gerard Pique wa Barcelona ahudhuria uzinduzi wa mkutano wa MWC

Kitu cha kuzingatia.

Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa komputa yako iwe na spidi ya prosesa iwe angalau 2.4GHz, RAM iwe na ukubwa wa kuanzia GB 4, na uwezo wa kuhifahi data (HDD) iwe ni kuanzia GB 250. Kwa wenye kompuyta yenye uwezo huu hawataona kero kutumia Windows 10.

Windows Vista haikupata mapokezi mazuri kwa watumiaji na ndio maana Microsoft wakaachana nayo na kuamua kutengeenza programu endeshaji iliyo rafiki na ambayo mpaka leo inapendwa.

Vyanzo: The guardian, dummies

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com