Jinsi Ya Kutoa Namba Yako Ya Simu Katika Hifadhi Ya TrueCaller!

0
Sambaza

TrueCaller bado inakuwa ndio chanzo bora cha kumgundua muwasilianaji kwa kutoa  jina au namba ya simu kwa kipindi cha muda wa miaka 6 mpaka sasa.

TrueCaller ni App nzuri sana ya kukuonyesha jina halisi la muwasilianaji wako na pia App hii inapatikana karibia katika kila soko la App za simu kama vile Google Playstore ya Android na AppStore ya iOs.

Japokuwa App ina sifa nyingi kuliko ubaya lakini inawezekana kuwa ukawa hupendi watu kuona au kujua namba yako pindi wanapotumia App hii basi hapo unaweza ukaiondoa kwa urahisi tuu.

SOMA PIA:  Facebook kudhibiti taarifa zinazochapishwa bila malipo

TrueCaller inakupa hayo mamlaka (ya kuweza kuondoa) na leo TeknoKona itaenda na wewe sambamba kuhakikisha unaweza fanya hivyo.

JINSI

TrueCaller inakupa mamlaka yote ya kuweza kufuta namba yako  katika hifadhi yake, unaweza fanya hivyo kiurahisha kwa kujitoa katika huduma hii kwa kutumia njia ifuatayo:-

Kwanza kabisa itakubidi u ‘deactivate’  (uipumzishe kwa muda) akaunti yako ya TrueCaller

Jinsi Ya Ku ‘Deactivate’

Fungua App ya TrueCaller katika simu janja yako

Nenda katika Eneo la ‘settings’ na kisha chagua ‘About TrueCaller’.  Ukiwepo hapo chagua ‘Deactivate Account’ na kisha bofya ‘Yes’. Ukifanya hivyo utakuwa umepumzisha akaunti yako ya TrueCaller kwa muda na unaweza ukaendelea katika kuifuta namba yako kabisa katika hifadhi ya TrueCaller …. Ngoja tuone njia

SOMA PIA:  Android Instant Apps: Tumia apps za Android bila hata kuzipakua (install)

Bofya link hii baada ya kuipumzisha akaunti yako ya Truecaller kwa muda

Sehemu Ya 'UnList' Katika TrueCaller

Sehemu Ya ‘UnList’ Katika TrueCaller

Weka namba yako ya simu ikianziwa na namba ya utambulisho wa nchi. Kisha Ingiza maneno/namba utakazoziona kwa lengo la kujua utambulisho. Sasa unaweza ukabofya ‘Unlist’ (yaani kujitoa kabisa)

Safi sasa namba yako itatolewa katika kumbukumbu za TrueCaller ndani ya masaa 24 na pia hakuna mtu yeyote ambae ataweza kukupata kwa kutumia TrueCaller  na pia hata wewe hutaweza kutumia TrueCaller ili kugundua watu mbalimbali – mpaka ujiunge tena –  Ni matumaini yabgu kuwa umeweza kufuta na kuiondoa namba yako katika hifadhi ya TrueCaller

SOMA PIA:  Skype yaingia mkataba na Paypal; sasa watumiaji wataweza kutuma pesa.

Kama unapitia tatizo lolote katika kufanya hivyo tuandikie sehemu ya comment hapo chini na sisi tutarudi tena kwako. Pia niambie kama njia hii imekusaidia. Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari moto moto za kiteknolojia. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com