Kutojibu "sms" kwasababisha mume kupewa talaka! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kutojibu “sms” kwasababisha mume kupewa talaka!

0
Sambaza

Kupuuza jambo fulani wakati mwingine unawza ukajikuta matatani pasipo kutarajia. Mwanamke mmoja nchini Taiwan ameruhusiwa kumpa talaka mume wake, kwa kutumia ishara kwamba ujumbe wake aliomtumia mumewe ulisomwa.

enter

http://gsredlon.com/ Mwanamke huyo alitumia mtandao wa kijamii wa Line unaonesha mumewe alikuwa akifungua ujumbe huo, lakini hakujibu. Katika ushahidi wa mlalamikaji ulionyesha alama za rangi ya bluu ambazo hutumiwa na mitandao kama vile Line na WhatsApp mtu anaposoma ujumbe kudai kwamba mumewe alikuwa ameupokea ujumbe.

Line ni mtandao unaoongoza katika mataifa kadha ya Asia

Kitendo cha mume wa mlalamikaji kutojibu sms anazotumiwa na mkewe halikuwa jambo ambalo lilitokea mara moja/mbili, mlalamikaji (mke) alimtumia mumewe ujumbe mara kadha, wakati mmoja ikiwa ni baada yake kulazwa hospitalini baada ya kuhusika katika ajali barabarani.

INAYOHUSIANA  Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi

see Soma pia: Kuachwa kisa tu kuchati

Katika ujumbe mmoja, alimwambia mumewe kwamba alikuwa katika chumba cha dharura hospitalini na akamwuliza ni kwa nini anasoma ujumbe wake lakini hamjibu. Ingawa mumewe alimtembelea hospitalini mara moja, mahakama ilisema kwamba hali kwamba alikuwa akipuuza ujumbe wake ni msingi tosha wa kumpa talaka.

Kwa muujibu wa Jaji aliyeamua kesi hiyo alijiaminisha kwamba kitendo cha mlalamikiwa kupuuza ujumbe aliotumiwa na mkewe huo ni ushahidi kwamba ndoa kati ya wawili hao haiwezi ‘kuokolewa’ na vyombo vingine hivyo akawaruhusu kupatiana talaka.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.