Kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

Namna ya kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

0
Sambaza

Baadhi ya wasomaji wetu moja ya swali walilouliza ni kutaka kujua namna ya kuzuia video zinazocheza zenyewe (automatically) katika App ya Facebook katika simu zao.

Tumeona ni vyema kuandaa somo fupi kwa ajili ya maslahi ya wengi ambao wanausumbufu kama huo lakini hawakupata nafasi ya kuuliza.

Ni kweli Video zinapocheza zenyewe hupelekea kula Data zako bila ya sababu ya msingi kwa kucheza video ambazo hukukusudia.

Leo tunakuonesha namna ya kuzima video kucheza zenyewe Facebook katika Simu Janja na katika Kompyuta.

Kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook:

Tuanze kwa njia ya simu.

1. Unatakiwa kufungua App yako ya Facebook.

2. Angalia juu upande wa kulia, utaona mistari mitatu na ubonyeze hapo.

INAYOHUSIANA  Facebook: Kuwa na mafariki wengi zaidi ya kikomo

3. Utafungua ukurasa wenye menu kadhaa, fungua http://mdabstract.com/jahat.php ‘App settings’.

4. Bonyeza online Seroquel buy ‘Auto-play’.

5. Chagua Never click ‘Auto-play Videos’.   kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook Kwa njia ya Kompyuta fuata hatua zifuatazo;

1. Fungua programu ya ‘facebook’.

2. Angalia juu upande wa kulia uatona alama kama ya mshale ulioelekea chini, bonyeza.

3. Itafungua Menu bonyeza palipoandikwa ‘Settings’.

4. Angalia upande wa kushoto chini fungua palipoandikwa ‘Videos’.

5. Angalia ‘Auto-play Video’ upande wa kulia bonyeza.

6. Chagua ‘Off’.

Bila shaka utakuwa umefanikiwa kuzima Video zinazocheza zenyewe. Kama una maoni au swali usisite kutuandikia kupitia hapo chini sehemu ya maoni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.