Kwa Kushangaza Kabisa, Pengine Hii Ndio Simu Ya Mwisho Ya Microsoft Inayotumia Jina La Nokia!

0
Sambaza

Nokia bado haijafa na ipo katika mchaka mchaka wa kuhakikisha kuwa inarudi tena, na wakati huu inakuja kwa kishindo ikiwa inaendeshwa na program Android.

Lakini tukiachana na hilo lingine la kushangaza limetokea, wengi walijua kampuni la Microsoft limesha achana na kuzalisha simu zenye jina la Nokia. Hivi karibuni limetangaza kutoa simu ambazo zina jina hilo.

Nokia 612

Nokia 612

Simu hizi zinategemewa kuwa ndio za mwisho kutoka Microsoft zikiwa na jina la Nokia. Simu hiyo inakwenda kwa jina la ‘Nokia 216’ na kwa mara ya kwanza itazinduliwa India.
Kmapuni limesema ujio wa simu hiyo mpya ni mzuri tuu licha ya kwamba karibia kila mtu kapagawa na ujio wa iPhone 7.

SOMA PIA:  Kivinjari cha Microsoft Edge kupatikana katika Android na iOS

Simu hii inakuja na kamera yenye MP 0.3 (kwa kamera ya mbele) na kamera ya nyuma inakua na flash. Simu hii kama kawaida itakuwa na FM redio. ‘MP3 player’ kwa ajili ya kucheza miziki na bila kusahau kuwa itakuwa na uwezo wa Bluetooth.

Nokia 612

Nokia 612

Ukiachana na hayo yote ni kwamba simu hii itakuwa inasapoti teknolojia ya 2.5G tuu katika swala zima la netiweki. Simu hii pia inakuja katika rangi tatu tofauti.

SOMA PIA:  Unsane: Filamu iliyorekodiwa kwa kutumia iPhone 7

Kama nilivyosema awali, hili bado ni jambo la kushangaza kwani kumbuka bado Mircosoft haijafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana katika soko la simu. Ukiangalia simu zao za Lumia na zile za Windows hazikufanya vizuri sana.

Nokia 612

Nokia 612

Simu hii itazinduliwa mwezi oktoba huko nchini India.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, wewe hii umeipokeaje? Je waachane na mambo ya simu kabisa?.

Tembelea TeknoKona kila siku kwani tupo mstari wa mbele kabisa katika kuhakikisha kuwa tunakuletea habari na mambo mengine yote yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com