Kutoka katika maandiko yaliyotoka ndani ya ikulu ya marekani (White House) ni kwamba sasa wananchi wanaweza wakatuma meseji kwa Raisi Obama.
Kwa msaada wa Facebook meseji hizo zitaweza mfikia Raisi Obama na yeye ataweza kuzisoma. Alikiri wazi kuwa meseji hizo huwa zinamsaidia katika mambo ya siasa, kujua nini kinaendelea na namna bora ya kuendesha nchi yake.
Raisi Obama alisema tangia aingie madarakani mwaka 2009 hii imekua ndio tabia yake, kwa siku lazima alikuwa asome barua kumi (10) kutoka kwa wananchi ambao wamemuandikia.Kwa sasa Facebook wameingilia kati na kurahisisha zoezi zima.
Hii Ndio Jinsi Ya Kutumia Meseji Muheshimiwa.
– Meseji hizi zote zitatumwa katika ukurasa wa Facebook wa Ikulu ya Marekani (The White House).
– Ukiwa katika ukurasa huo, unaweza ukachagua sehemu ya Meseji ambapo kitatokea kiboksi kama kawaida cha kuandika.
– Ukishamaliza kutuma meseji yako, itatokea meseji nyingine ikikuuliza baadhi ya maswali kama vile E-mail yako (Kama raisi atakujibu barua pepe yako inaweza ikatumika)
Ukiachana na hayo yote, kitendo tuu cha Facebook kuwezesha raia kuweza kumtumia meseji Raisi Obama inaonyesha ni jinsi gani mambo yanabadilika na kwa jinsi gani teknolojia inachangia katika mabadiliko hayo.
Je unahisi huduma kama hii kwa Tanzania itawezekana? Ningependa kusikia kutoka kwako Niandikie sehemu ya comment hapo chini.
Mawasiliano mema na Raisi Obama ila Usiombe hela tuu Hahahaah!