Kwa Ufupi: Habari Mseto za Wiki!

0
Sambaza

Kuanzia sasa tutakuwa tunakuleta ‘Kwa Ufupi: Habari Mseto za Wiki!’ kila mwisho wa wiki tukikupa habari mbalimbali kwa ufupi ambazo hatukufanikiwa kuaziandika katikati ya wiki!

Soma, i’tweet, ipe ‘Like’ na tuma kwa wengine..usisahau ku’Like’ ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/teknokona

Mwamvita Makamba ala shavu Afrika Kusini, sasa kufanyia kazi makao makuu!

 

Mtoto wa Mzee Yusuf Makmba na mdogo wa Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, na vilevile aliyekua Chief officer: Marketing and Corporate Affairs katika kampuni ya Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba amehamishiwa kwenye ofisi ya makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo nchini Afrika Kusini.Ametoa taarifa hiyo alhamisi kupitia mitandao ya Twitter na Facebook.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Block Simu Katika iOs Bila Ya Kutumia App! #iPhone

Chanzo: Bongo5

Kampuni ya RIM Watengenezaji Wa Simu Za Blackberry Waanza Kampeni za Simu Zao Mpya!

 

Kampuni ya RIM imeanza kuonesha makampuni ya mawasiliano duniani simu zake za Blackberry 10 ikiwa ni matayarisho ya kuzileta simu hizo ndani ya miezi michache baadaye. Watafiti wengi wanasema simu hizo zitaweza ingia sokoni mwanzoni mwa mwakani.

Kampuni ya RIM ipo katika wakati mgumu kifedha, watu wa Amerika ya Kaskazini (Marekani na Canada) wengi wameachana na simu za Blackberry wakipendelea simu zenye mvuto za Android na iPhone, hivyo simu hizi mpya zitakazokiwa zinatumia programu mpya ya Blackberry 10 ndio kama kamba itakayoweza kuiokoa kampuni hii.
Chanzo: http://ibnlive.in.com/news/rim-begins-showing-new-blackberrys-to-carriers/285044-11.html

Apple Yashinda Kesi Marekani Dhidi ya Samsung, Nchini Korea Wote Waadhibiwa!

Kampuni ya Apple imeshinda kesi dhidi ya kampuni ya Samsung ambapo kampuni hiyo ilidai fidia dhidi ya kampuni ya Samsung kwa kile wanachodai simu ya Samsung Galaxy SII kuiba muonekano wa simu za iPhone. Hivyo Huko nchini Marekani kampuni ya Samsung imetakiwa kuilipa Apple Dola za Kimarekani Bilioni moja. Kesi nyingine iliyofikishwa nchini Korea kusini kampuni zote mbili zilikutwa na hatia ya kuibiana teknolojia na hivyo zote kutakiwa kulipana, inategemewa kesi hizi zitafunguliwa katika masoko mengine makubwa duniani.

SOMA PIA:  Pixelbook: Kompyuta ya kwanza kutoka Google yenye 'Kisaidizi binafsi'

 

Apple walishafungua kesi nchini Uingereza wakidai kampuni ya Samsung imeiga ubunifu wa iPad katika kutengeneza Samsung Tab tableti, lakini mahakama ya uingereza ikatolea nje madai hayo na kuitaka kampuni ya Apple ifanye kampeni ya matangazo ya kusafisha jina la Samsung.

 

Kaa tayari kwa habari zaidi kuhusu muenendo wa kesi hizi.

 

Gharama za Huduma za Blackberry Zazidi Kushushwa!

 

Makampuni ya simu Tanzania yazidi kupunguza gharama za huduma za Blackberry, hii ni habari nzuri kwa watumiaji wa simu za blackberry, lakini swali je vipi kuhusu watumiaji wa intaneti wa kompyuta? Nadhani huku nako kunaitaji ushindani kwani bado gharama zipo juu.

SOMA PIA:  Samsung kuuza simu za Galaxy Note 7 tena, kwa bei nafuu!

 

Tunakutakia Jumapili Njema!

Facebook Comments
Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com