Kwanini Upakue Programu ya 365Scores?

0
365-scores

365Scores

Je, wewe ni mshabiki wa mpira wa miguu au michezo mingine kama mpira wa kikapu na tennis? Kama jibu ni ndiyo, basi utaipenda programu ya 365Scores.

Hii ni programu za kitumi cha mkononi itakayokuletea habari, itakayo kukumbusha kuhusu mechi punde itakapoanza, kukujulisha yenyewe punde goli la timu unayofuatilia litakopingia, mtu atakapopewa kadi na hata kukujulisha pale mchezaji anaponunuliwa rasmi na klabu unayoipenda. Unaona raha hiyo? Huna haja ya kutafuta habari. Habari zinakufuata. Zaidi ya yote, 365Scores itakuletea video za magoli yaliyofungwa kwenye mechi za timu unazofuatilia.

Kupata huduma hii, basi huna budi kuingia playstore na kuipakua programu ya 365Scores na kuiweka kwenye kitumi chako. Kisha unafanya chaguzo kadhaa kuhusu kujiunga, michezo, timu na mataifa unayotaka kufuatilia. Kisha unaanza kutumia.

Programu hii inapendwa sana na watu tofauti duniani ila tatizo moja linaweza kuwa iko slow kidogo kwenye vitumi vyenye uwezo mdogo hadi wa kati ila vinginevyo, 365Scores ni programu bomba kwa ajili ya wewe mdau wa michezo.

Umejaribu programu hii? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com