‘LapTops’ motomoto za Windows 8 zanukia..Kitu cha Asus

0
Sambaza
Najua wengi wetu tushasikia kuhusu Windows 8 ambayo inategemewa kutoka rasmi mwishoni mwa mwaka huu….sitaandika mengi kuhusu hili kwa sababu makala maalumu kwa ajili ya Windows 8 ipo jikoni, kwa hiyo usisahau kurudi tena.
Ila ningependa kuandika kuhusu laptop inaytengenezwa na kampuni ya Asus, laptop hiyo itakayoingizwa sokoni ikiwa na Windows 8 ni ya kipekee sana. Tarehe rasmi ya kuwa sokoni bado ijatolewa ila lazima itakuwa baada ya Windows 8 kutoka rasmi mwishoni mwa mwaka huu. Na itaitwa Asus Taichi!

 
ANGALIA VIDEO HII WAKIIONESHA
Laptop hiyo itakuwa na ‘screen’ mbili, ya mbele na nyuma. Utaweza kuwa unafanya kazi nyingine kama kuandika taarifa zako muhimu upande mmoja, wakati unaweza kumuwekea mama watoto/watoto kideo kwa upande mwingine. Na upande wa nyuma upo ‘touch screen’, tunaelewana? yaani unaweza kufanya mambo kwa nguvu ya kidole chako tuu, yaani ni ‘tablet’. Unaweza zima mbele, ukafunga laptop yako afu ukawa unaitumia kama ‘tablet’ upande wa juu, yaani mtu wa IPad, Galaxy tab, hawakuambii kitu…. so ni ile kitu watu wanaita ‘two in 1’. Ku’skype kwa sana kwa sababu kitu kina kamera pande zote mbili.

Kwa wale watu wa ma’specifications ni kama ifuatavyo screen mbili nyuma na mbele za inchi 13.3, pia unaweza pata ya inchi 11.6 (IPS HD displays), an Ivy Bridge Core i7 processor, RAM ya 4GB , SSD storage(pa kusomea kadi zile ndogo za camera), USB 3.0 ports mbili, Micro HDMI, mini DisplayPort, a 5-megapixel rear camera, and “HD” front-facing camera.
Kaa mkao wa kula, tutaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusu Windows 8 na vifaa vipya vya Windows 8!
Umekinaje hichi kitu? Je ukiwa na mshiko utakinunua? Kwani utavunja bajeti ya laptop na tablet….lakini je kitadumu kibongo bongo? #daladala
Facebook Comments
Sambaza
SOMA PIA:  Acer Watangaza Matoleo Mapya Ya Tabiti (Tablet)!
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com