Leo ni miaka 10 ya Hashtag – #, unajua nini maana yake?

0
Sambaza

Siku ya leo inatimia miaka kumi tangu Hashtag ya kwanza kutumiwa na mtaalamu wa mitandao ya kijamii, Chris Messina katika mtandao wa Twitter. Hashtag ya kwanza ilitumwa mwaka 2007 Agosti 23.

Hashtag hiyo ilikuwa kwa ajili ya kukusanya majadiliano na maongezi yote ya kampuni ya Barcamp #Barcamp.

Kabla ya mtandao wa kijamii wa Twitter watu wengi hawakujua matumizi wala ukweli kuhusu Hashtag iliyo kwenye Keyboard.

Mtandao wa Twitter ulibadilisha matumizi yake na kuifanya Hashtag kuwa kitu muhimu kwa jamii.

SOMA PIA:  Uber na Tigo zashirikiana kama njia ya kuwafikia wateja wao vizuri

hashtag

Asili na Matumizi yake

Historia ya Hashtag haipo wazi sana ila kwa mujibu wa mitandao kadhaa imetokana na neno ‘Tag’ na lilivumbuliwa na watu wa mtandao wa Twitter.

Hashtag imeundwa na watumiaji wa mtandao ili kujadili matukio maalumu na masula husika kwa wakati muafaka.

Na nji hii husaidia kwa makusudi yaliyopangwa ili watumiaji wengine wa mtandao waweze kutafuta kwa urahisi mada na kushiriki katika mazungumzo bila ya kujali wapi duniani.

Hii ndio Hashtag ya kwanza

Katika wakati wa nyuma Hashtag ilikuwa ikitumika kwenye Internet Relay Chat (IRC) katika mfumo wa zamani wa kuchati uliokuwa ukitumiwa na makampuni mbalimbali.

SOMA PIA:  Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa Twitter Evan illiams anasema yeye na Chris Messina hawakuwahi kufikiria kwamba hashtag itakuja kuwa maarufu kama ilivyo sasa kwa sababu ilikuwa ikitumika na wataalamu wa mfumo wa IRC.

Vituo vingi vya Televisheni duniani vimekuwa vikitumia hashtag kwa ajili ya kuwaongoza watazamaji wao kuelekea mazungumzo ya mtandaoni, kujadili mada iliyowekwa na kuchangia.

Aidha, Jukwaa la vyombo vya habari la kijamii linaashiria kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 10 ya hashtag kwa  #Hashtag10.

SOMA PIA:  Viongozi wa makundi WhatsApp 'kuongezewa nguvu'

Kwa sasa Hashtag inatumika na mitandao kadhaa zaidi ya Twitter na watu wengi wamekuwa wakiifahamu. Je msomaji wetu ushawahi kushiriki mjadala wowote kupitia hashtag. Au ushawahi kuona hashtag? Tupe maoni yako.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com