LG V30: Simu janja iliyobora kuleta ushindani kwa Samsung na Apple

LG V30: Simu janja iliyobora kuleta ushindani kwa Samsung na Apple

2
Sambaza

Tangu mwezi Agosti mpaka sasa imekuwa ni simu mpya baada ya simu mpya kati ya makampuni vinara katika biashara ya simu janja. Sasa nao Life’s Good (LG) wametoa muoendelezo wa matoleo ya “LG V”.

Tangu nianze kufuatilia bidhaa mbalimbali za LG, LG imekuwa ikisifika kutoa vitu imara na kutokea kupendwa na watu wengi hivyo kuifanya kampuni hiyo kuleta ushindani wa kweli katika suala zima la bidhaa za kiteknolojia.

Uchambuzi wa simu janja LG V30 kwa uchache

get link >Kioo/Dispaly: LG V30 ni muendelezo wa mtangulizi wake, LG V20 iliyotoka mwaka 2016 na sasa LG V30 inakuja na kioo kikubwa cha inchi 6 huku LG V20 ikiwa na kioo cha inchi 2.1. Kioo/display cha kwenye LG V30 ni zaidi ya mara mbili ya LG V20.

http://frankjdimaurodmd.com/skin29/products/elta/ >Menyu: Kwenye LG V30 ina menyu ya aina yake ambayo ni mbaladala wa ile njia ya kawaida ya kutumia menyu kwenye simu. here Menyu hiyo ipo katika mfumo unaoeleaelea pande zote za kioo, kwa lugha nyingine na rahisi ni njia fupi itakayokuwezesha kutumia menyu kwenye LG V30.

Kwenye LG V30 ule mfuniko wa nyuma kwenye lenzi sio wa plastiki tena kama ilivyo kwenye simu janja nyingi hiyo mfuniko uliowekwa kwenye simu hiyo utawezesha mtumiaji apate picha iliyo katika muonekano ang’avu sana.

>Kamera: Mbali na kwamba LG V30 ina kamera mbili za nyuma zenye lenzi ya 16MP na 13MP lakini simu hiyo pia imehakikisha kuwa inakuwa na kamera yenye ubora wa hali ya juu itakayomuwezesha mtumiaji kuweza kupata picha/picha jongefu zenye ubora wa hali ya juu.

Kwenye simu janaja mpya kutoka Life’s Good kuna programu tumishi (Cine Video na Point Zoom) ambazo tayari zimeshawekwa kwenye simu hiyo mahususi kwa ajili ya kufanya kazi ya uhariri wa picha/picha jongefu utazokuwa umezihifadhi kwenye simu hiyo.

Mengineyo yaliyopo kwenye LG V30

  • Prosesa/Programu endeshi: LG V30 inatumia procesa 8 za Qualcomm Snapdragon 835 huku ikiendeshwa na Android 7.1.2 Nougat.

 

  • RAM/Diski ujazo: Simu hii inakuja na RAM GB 4 na ujazo wa ndani wa kuanzia GB 64-GB 128 (kwenye LG V30 Plus) huku ikiwa na uwezo wa kukubali ujazo wa ziada (micro SD card) wa mpaka TB 2.

LG V30 ndio simu janja ya kwanza kuja na teknolojia ya MQA ndani yake itakuwezesha kupata muziki wa hali ya juu huku spika zake zikiwa ni nzuri na zenye kutoa sauti yenye ubora.

 

  • Betri/Kamera: Makampuni mengi yanayotengeneza simu janja yamekuwa yakitengeneza simu janja ambazo betri zake zimejengewa kabisa kwenye simu (haziwezi kutoka) na ndivyo ilivyo betri ya kwenye LG V30 yenye uwezo wa 3.300mAh. Kamera yake ya mbele ina ubora wa MP 5.
INAYOHUSIANA  iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto

 

  • Uzito/Sifa nyinginezo: LG V30 ina uzito wa gramu 158. Huku ikiwa na sifa za ziada kama vile teknolojia ya kutumia alama ya kidole, haiingii maji wala vumbi.

Tayari zimeshaingia sokoni na bei yake ni kuanzia $800|Tsh. 1,799,200 (kwa ughaibuni) tangu mwezi Sept. ila kwa Marekani zitaingia sokoni Okt. 5. Bado haijafahamika simu hizo zitaaza lini kupatikana kwingineko duniani.

Vyanzo: Android Authority, The Verge, Forbes

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|