LG wanarudi vizuri kwenye biashara ya simu; Wapata faida baada ya miaka mingi ya hasara

0
Sambaza

LG ni moja ya makampuni nguli ya muda mrefu zaidi katika sekta ya vifaa vya elektroniki. Na baada ya miaka mingi ya kitengo chake cha simu kufanya vibaya kimauzo sasa kimerudi kwenye mafanikio.

lg electronics lg wanarudi

LG Electronics ni kampuni ya nchini Korea Kusini, ilianzishwa mwaka 1958

Miaka ya mwanzoni ya simu janja (smartphones) simu za LG zilibeba sifa za ubora na upekee wa hali ya juu tuu, ila inaonekana ushindani ulivyozidi kukua katika sekta hii kuna makosa yalifanyika na wakajikuta kitengo hicho cha biashara mauzo yake kushuka na kufikia hali ya kutengeneza hasara.

SOMA PIA:  Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

Mwaka wote wa 2016 kitengo hicho kilitengeneza hasara lakini katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu kitengo hicho kimetengeneza faida.

Kampuni ya LG Electronics inaamini mafanikio yao yamechangiwa na toleo lao la simu ya LG G6 pamoja na zingine kadhaa zinazolenga watumiaji wa aina zote.

LG G6

Muonekano wa LG G6

Kumekuwa na ukuaji mkubwa wa idadi ya simu walizoingiza sokoni – waliingiza simu milioni 14.8, ambao ni ukuaji wa asilimia 10 (wa mwaka hadi mwaka). Wakiwa na mauzo ya takribani dola bilioni 5.12 (Zaidi ya Trilioni 11.4 za Kitanzania) ambao ni ukuaji wa asilimia 8.8. Faida nyingi ikiwa imetokana na mauzo nchini Marekani.

SOMA PIA:  Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja Ifikapo 2020, kushirikiana na LG!

Soma uchambuzi wa simu ya LG G6 – Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

Je una mtazamo gani juu ya simu kutoka kampuni ya LG?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com