Simu rununu zipo na zinatoka kila leo na hii inadhihirika kwa kampuni mengi kama hawajatoa tayari simu mpya mwezi huu basi wapo njiani kutoa bidhaa kwa ajili ya wateja waliopo sehemu nyingi duniani.
Life’s Good (LG) ni moja ya makampuni ambayo yapo kwenye biashara ya vifaa vya kiteknolojia kwa miaka mingi tu na tukizungumzia simu janja basi watu wengi tu watakuwa wanafahamu/wameshawahi kutumia simu mbalimbali za LG.
Mwezi Mei 2018 LG wametoa simu janja, LG K30 ambayo ni simu yenye muonekano mzuri iliyojidhatiti zaidi kwenye upande wa diski uhifadhi.
LG K30 ni simu rununu ambayo haina sifa lukuki lakini inafaa sana kwa yeyote yule ambaye anahitaji kuwa na simu janja ambayo imekamilika kila idara kuanzia kasi ya intaneti, uzito na uwezo wake wa kuhifadhi vitu.
Simu janja mpya kutoka LG ina sifa zifuatazo:-
Kioo: Ukubwa wa inchi 5.3 ambacho ni cha mguso na ubora wa muonekano wa picha ni 720*1280pixels,
Prosesa: Kasi ya prosesa ni 1.4GHz quad-core Snapdragon 425 SoC ikiwa inatumia Android 7.1 Nougat,
Betri: Betri yake ina 2880mAh inayokubali teknolojia ya kuchaji simu haraka,
Diski uhifadhi/RAM: LG K30 ina nafasi ya GB 32 kuhifadhi vitu kwenye simu na kuweza kukubali memori kadi ya mpaka TB 2. RAM yake ni GB 2,
Kamera: Kamera ya mbele ina MP 5 na ile ya nyuma ina MP 13 yenye uwezo wa kurekodi video katika kiwango cha 1080p,
Mengineyo: Inatumia teknolojia ya alama ya kidole, uzito wake ni gramu 168, 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, na GPS/ A-GPS vipo kwenye LG K30.
Unapenda simu janja za LG? LG K30 sasa ipo kwenye mipango yako ya simu ambayo utainunua? Tunakaribisha maoni yako.
Vyanzo: Gadgets 360, Android Authority
One Comment
Comments are closed.