LibreOffice: Programu Mbadala Kwa Microsoft Office!

0
Sambaza

Kama unaandika nyaraka yeyote (document) au unatengeneza kitu cha kukielezea au hata kama unapangilia baadhi ya vitu vyako vya kila siku kuna hati hati kubwa unafanya hivyo kwa kutumia ‘Microsoft Office’.

Microsoft Office bado ni baba wa yote hayo katika ‘Software’ za kufanyia kazi mbalimbali. Lakini hata hivyo bado MS Office ipo katika upande ambao unachukua kiasi Fulani cha pesa yako. Yaani kuipata kwake itabidi mtu alipie ili aweze kupata leseni ya kutumia.

Pia kama una toleo la zamani ambalo halifanyi kazi vizuri kwa sasa au kompyuta ambayo haina Ms Office hapo tena itakuwa ni shida kwani itakubidi utumie mfuko wako kuhakikisha kuwa unapata toleo jipya.

Sasa yote ya nini hayo? Unaweza ukapata programu ya Office sawa yenye nguvu na uwezo kama Ms Office bila ya kufungua mfuko wako

SOMA PIA:  Ondoa tatizo la mafaili katika flashi kuonekana kama Shortcut

Ndio bila ya kufungua  mfuko wako!  Kwa kutumia LibreOffice hilo linawezekana. Kama hujawahi kuisikia hapo mwanzoni LibreOffice ni programu ambayo inaendana na Ms Office. Pia programu hii inapatikana wazi wazi (Open Source) na pia mara kwa mara inafanyiwa maboresho na kitu kizuri zaidi ni kwamba ni ya bure kabisaaaaaaaaaa!

LibreOffice inatoa programu 6, zile ambazo zitatoa huduma ambazo unazijua kama umeshawahi kutumia Ms Office ni Writer, Calc, na Impress ambazo ziko sawa tuu na Microsoft Word, Excel, na PowerPoint. Kwa kiasi kikubwa hizi zina vipengele vinavyofanana tuu inakuhitaji tuu kuzunguka zunguka ili kuvipata.

LibreOffice

LibreOffice

Kizuri zaidi ni kwamba LibreOffice ina uwezo wa kufungua na kuhariri faili ambalo umelitengeneza kupitia ‘Ms Word’ na ikalisevu kama file la ‘Office’.

SOMA PIA:  Namna ya kuweka Play Store katika simu zenye mfumo wa kichina

Pia ina uwezo wa kufungua mafaili mengi tuu ukiachana na yale ya Ms Word pia mafaili kama ya ‘OpenDocument Format’ (ODF) na PDF yanaweza yakafunguliwa bila shida.

Jinsi Ya Kushusha Na Kupakua

Ili kushushua programu hii kwanza inakubidi uende katika mtandao wa LibreOffice katika sehemu yake ya kushusha (download). Ukifika katika upande wa kushoto kuna eneo la kushusha lenye ukijani na limeandikwa “Download Version X.X.X

Ukibofya hapo itaanza kushuka haraka iwezekanavyo. Na pia kwa sababu LibreOffice ni programu ya watu kwa ajili ya watu, wanaoimiliki watakuomba kuchangia kidogo lakini kama unataka kufanya hivyo. Kama hutaki kuchangia utaendelea tuu kushusha programu hiyo.

Kushusha kukikamilika  fungua na anza kupakua programu hiyo. Kumbuka program hii itakuomba tuu uchangie (unaweza ukakataa), ukiona inakuomba malipo sitisha kupakua kwani unaweza ukawa umefungua ‘Link’ ambayo sio sahihi.

SOMA PIA:  Uwezo wa kurudisha kile kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye memori ya simu

Pia kumbuka hii ni programu kubwa kwa hiyo itachukua muda kidogo katika kujipakua katika kompyuta yako. Programu ikimaliza kujipakua unaweza ukaifungua kwa kutumia ‘Shortcut’ iliyojitengeneza katika skrini ya kompyuta yako.

Kwa urahisi Fungua Link Hizi Na Ushushe Moja Kwa Moja

Shusha Kwa Windows  – Bure

Shusha Kwa MacBure

Baada ya hapo ni matumaini yangu kuwa hauitakuwa ukitegemea programu za ‘word’ tuu katika kufanya kazi zako mbalimbali. Niandikie sehemu ya comment hapo chini hii umeipokeaje. Usiache kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com