LinkedIn ni mtandao wa kijamii, tena namba moja kwa wataalamu wa sekta fulani fulani. Kampuni imeamua kuja na orodha ya makampuni ambayo watu wametuma maombi mengi ya kazi.
Kumbuka pia LinkedIn ni mtandao wa kijamii ambao unatumiaka kama uwanja wa kutangaza ajiri kwa makampuni ambayo yana uhitaji wa wafanya kazi.
Makampuni Haya Ndio Yaliyofurikwa Na Maombi Ya AJira Kwa 2017!
- ALPHABET
kampuni ya kwanza kabisa linaloongoza kwa kupokea maombi mengi ya kazi ni ALPHABET ambayo inamiliki kampuni ya Google. ALPHABET imejikita katika mambo mbali mbali ya teknolojia. Google kwa haraka haraka ina wafanyakazi zaidi ya elfu 57,100
2. Amazon
Hii imechukua nafasi ya pili kwa kupata maombi mengi ya ajira katika mtandao wa kijamii wa LinkedIn. Vile vile kumbuka Amazon ndio mtandao wa kwanza unaopata mapato mengi kuliko mtandao mwingine wowote duniani katika makampuni yanayohusisha Intaneti.
3. Facebook
Pengine wengi labda walizani Facebook itachukua namba moja au mbili kwa umaarufu wake. Imeangukia namba tatu pia facebook ni moja kati ya mtandao mkubwa sana duniani. Ni namba moja katika mitandao ya kijamii na hii ni kwa umaarufu na kimapato
4. Uber
Hili ni moja kati ya makampuni ambayo yamekua kwa kasi ya ajabu na yakaamua kujitanua duniani kote haraka iwezekanavyo. Hawa wamefika mpaka Tanzania, japokua kampuni limekua likipata majanga ya mara kwa mara lakini hilo pekee halijafanikiwa kuliweka kampuni chini ya orodha.
5.Tesla
Moja kati ya makampuni maarufu sana ya kutengeneza magari ya umeme. licha ya hivyo hii sio kampuni ya kutengeneza magari tuu lakini inajikita pia katika nishati. Hivi karibuni Tesla imejipatia jina kubwa na kupiga bao makampuni kama vile Ford.
6. Apple
Ni wazi kuwa lazima katika listi hii kampuni la Apple liwepo sio? ndio kampuni linaloongoza katima makampuni yale yanayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa simu na teknolojia nyingine. Apple wako vizuri na dunia nzima inalijua hilo, hii inaweza ikawa sababu tosha juu ya kwanini watu wanatuma maambi mengi ya ajira katika kampuni hilo.
7. Time Warner
Hii ni kampuni ambayo inajihusisha na mambo ya ‘Media’ na mambo mengine. licha ya kuwa na sifa mbaya katika utoaji huduma lakini bado imefanikiwa kwa kiasi fulani kufikia mpaka namba saba.
8. Disney
Ni kampuni iliyojitosheleza kabisa na ina bishara nyingi. kwa mwaka jana ndio kampuni ambayo ilikua inaongeza kwa usambazaji wa filamu. Filamu nyingi zilizosambazwa na kampuni hii zilizidi mauzo ya dola bilioni moja za kimarekani. licha ya hivyo bado ina vipindi wa Tv ambavyo vinafanya vizuri sana.
9. NBCUniversal
NBCUniversal na yenyewe haina tofauti kubwa sana na Disney ni vile vile tuu yote yanajihusisha na mambo ya ‘Multi-Media’.
10, SalesForce
Hii ndio imeshangaza wengi baada ya kuingia katika listi hii. Kampuni hii inajikita katika utengenezaji wa ‘software’ mbalimbali. Kingine kikubwa kuhusu kampuni hii ni kwamba inawajali sana wafanya kazi wake, kwa kuwapa marupu rupa na kipaumbele cha kutosha. Pengine hili linaweza likiwa ni moja ya jambo ambali linaifanya kampuni ikimbiliwe
Hizi ndio kampuni zinazoongoza kupokea maombi ya kazi kwa kupitia mtandoa wa kijamii wa LinkedIn ambao kwa sasa unamilikiwa na kampuni ya Microsoft.