Live video kuja Instagram.

0
Sambaza

Kumezuka tetesi kwamba mtandao wa Instagram upo mbioni kuleta live video kwa watumiaji wake, huduma hii ambayo tayari ipo katika mitandao mingine kama vile Facebook Twitter na Youtube.

Mtandao wa Financial Times umeripoti habari hii baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Instagram.

live video

Screenshot kuonesha huduma mpya ikiwa katika majaribio

Akiongea na mtandao wa Financial Times Mkurugenzi mkuu wa Instagram Kevin Systrom amesema kwamba video za live ni kitu ambacho kinawasisimua na wanaangalia namna ambavyo itaweza kuboresha huduma zao.

SOMA PIA:  Google yafanya mabadiliko muonekano wa tovuti yake katika simu janja

Mwanzilishi wa Facebook hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba kampuni ya Facebooka mbayo pia ni wamiliki wa  Instagram na Whatsapp yatazipa video kipaumbele katika utoaji huduma wake, hii inazidi kuthibitisha tetesi hizi ambazo zimesambaa mitaani.

ntfhytq1mgrinymvul9wd2ntum9sbvbha044by1hy1hmmklumdlrps84ohg0nzc6nty3mngzmzyzlzeyodb4njiwl2zpbhrlcnm6cxvhbgl0esg3nskvahr0chm6ly9z

Tayari Instagram ilikwisha leta kipengere cha Stories ambacho kiliigwa kutoka katika mtandao wa Snapchat na baada ya  kuleta kipengere hicho Instagram imepata mafanikio makubwa na pia wiki hii kipengere hichi kimeboreshwa zaidi.

SOMA PIA:  Utafiti: Mitandao ya kijamii chanzo cha habari kikubwa kwa watu wengi

Live video tayari imekuwa na mafanikio katika mitandao mingine kama Facebook Twitter na Youtube ambao uliweza kupata ongezeko la asilimia 80%ya watumiaji ambao waliangalia live video mwaka huu.

Je wewe unaangalia video live video katika mitandao ya kijamii? tuandikie katika sehemu ya maoni.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com