M-Safiri; App inayokuwezesha kupata tiketi bila kupanga foleni

0
Sambaza

Hakuna mtu anayependa kwenda sehemu kwa ajili ya kununua tiketi halafu ukatumia muda mrefu kununua tiketi yako ili uweze kusafiri. TeknoKona imekuja na utatuzi wa adha hiyo.

App inayotambukiwa kwa jina la M-Safiri imetenezwa na wanafunzi wa sekondari nchini Kenya, Precious Blood na Riruta wanaofahamoka kama “Team Sniper” walishika nafasi ya pili katika shindano la “Technovation Challenge 2016” lililofanyika San Francisco, California-Marekani.

App hiyo ni mahususi kwa kurahisisha ununuzi wa tiketi za usafiri, kwa magari ya masafa marefu na programu hii inakuongoza hadi kwenye kituo cha basi kwa kutumia teknolojia ya kugundua maeneo (GPS). Badala ya kwenda kupanga foleni, utaenda tu kupanda gari moja kwa moja.

App ya M-Safiri inakuwezesha kukata tiketi ya kwenda safari bila kupanga foleni kpata huduma.

App ya M-Safiri inakuwezesha kukata tiketi ya kwenda safari bila kupanga foleni kpata huduma.

Sababu ya kutengeneza M-Safiri

Harriet Karanja, 16, alikuwa kwenye foleni akisubiri kununua tiketi ya kusafiri kwa basi jijini Nairobi, wakati mama mmoja aliyekuwa kwenye foleni alipokonywa mali yake na wezi na aliposimulia tukio hilo kwa wenzake wanne shuleni, aligundua kwamba pia wao walikuwa wameshuhudia tatizo sawa na hilo. Itakuwaje iwapo tutabuni njia ya kuwaondoa watu kwenye foleni kununua tiketi?

SOMA PIA:  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Wasichana hao walipata usaidizi zaidi kutoka kwa walimu, wakufunzi, washauri pamoja na kampuni ya simu ya Safaricom ya nchini Kenya. Baada ya kumaliza masomo yao wasichana hao wana mpango wa kufungua kampuni yao ya teknolojia baada ya masomo ya shule ya upili (sekondari), na pia wanapanga kuisajili programu yao na kuiweka kwenye soko la programu za simu.

Team sniper waliibuka nafasi ya pili katika mashindano ya kutengeneza programu za simu nchini Marekani

Team sniper waliibuka nafasi ya pili katika mashindano ya kutengeneza programu za simu nchini Marekani

Awali wasichana hao walikuwa hawajui jinsi ya kutengeneza programu hizo, kuandika mpango wa biashara ama kuandaa na kuwasilisha wazo la kibiashara.

Lengo kuu likiwa ni kuwapa hamasa wanawake kujiingiza katika masuala ya teknolojia ikiwemo uundaji wa apps mbalimbali na kuongeza motisha kwa watu hasa wanawake kujiajiri. Je, unadhani ni kwa kiasi gani app hiyo itapunguza/kumaliza adha ya kupanga foleni wakati wa kununua tiketi?

Vyanzo: BBC, kachwanywa.com

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com