Katika hali ya kawaida tumukuwa tukinunua bidhaa za Apple (iPhone, iPod, n.k) ambazo tangu zianze kuuzwa zimekuwa zikisifiwa na hata kufanya vizuri kimauzo. Lakini kitu ambacho wengi hawajui ni maana ya “i” kwenye bidhaa hizo.
Bidhaa za kama iPhone, iPad na nyinginezo ni vitu ambavyo basi katika yale matamanio ambayo kama mpenda teknolojia basi siku utakayiweza kumiliki iPhone utajisikia faraja sana kwani kila mtu anapenda vitu vizuri na ni ukweli usiopingika kuwa bidhaa za Apple ni za aina yake.
Historia ya “i” kwa ufupi
Chimbuko la “i” kwenye bidhaa za Apple zilianza mwaka 1997 wakati ambapo marehemu Steve Jobs alirejea kwenye kampuni (Apple) ingawa hakutaka kuwa mwajiriwa ila alirudi kama “Kibarua” tu na “i” ilianza kuonekana kwa mara ya kwanza kabisa kwenye iMac.
Wakati kompyuta hiyo inazinduliwa, mwanzilishi wa kampuni hiyo Steve Jobs alisema kompyuta hiyo imetengenezwa mahususi kwa watumiaji wa mtandao (internet), kwani kipindi hicho ndio kilikuwa kipindi ambacho teknolojia ya mtandao (internet) kimeanza kushinda nyoyo za watu wengi na ndiyo ilikuwa kitovu cha biashara kupitia kompyuta.
Kwenye uzinduzi wa iMac aliyekuwa nguli katika masuala ya teknolojia, Steve Jobs aliweka wazi maana ya herufi “i” kweneye iMac ambayo ni Internet, individual, instruction, inform, inspire na mengineyo.
2 Comments
Comments are closed.