Wakazi katika miji mitatu mipya nchini Singapore watakuwa wa kwanza kupanda mabasi ya abiria yasiyo na dereva kama sehemu ya safari zao za kila siku kuanzia mwaka wa 2022.
Waziri wa miundombinu wa Singapore Bw. Khaw Boon Wan wakati wa ufunguzi wa jaribio la basi la kwanza lisilokuwa na dereva nchini humo, ametangaza kuwa kuanzia mwaka 2022 mabasi hayo yataingia barabarani kufanya kazi ya kusafirisha abiria.
Ripoti zinaonyesha kuwa huenda miaka mitano ijayo wakazi wa miji tofauti nchini humo wakapendelea zaidi kutumia mabasi yasiyokuwa na dereva kwa ajili ya kwenda makazini pamoja na kukuza maendeleo katika miji hiyo kutokana na uwepo wa mabasi hapo.