Maboresho: Instagram Direct yazidi kunogeshwa .

0
Sambaza

Instagram Direct ambayo ni huduma ya ujumbe ndani ya mtandao wa Instagram imefanyiwa maboresho kadhaa wiki hii, maboresho haya yanalenga kuipa Instagram Direct uwezo kama ilivyo kwa mitandao mingine ambayo inatoa huduma za ujumbe na kuchati.

buy Dilantin mexico

where can you buy herbal viagra Direct

Makala hii itayaangalia mabadiliko makubwa ambayo yamekuja na maboresho hayo kama ifuatavyo;-

Uwezo wa kupata muhutasari wa Link unazotuma.

Tangu kuanzishwa kwake mtandao huu ulikua hauruhusu kuona muhutasari wa link ama viunganishi unavyo tumiwa na marafiki, jambo hili lilikuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa mtandao huu hasa ukizingatia tayari jambo hili lilikuwa linapatikana katika mitandao mingine mingi. Kuletwa kwa muhutasari wa viunganishi kunaileta Insta direct katika anga za app nyingine za namna hii na pia unawapa uwezo watumiaji wake kufanya mambo mengi ndani ya app bila ya kutoka.

direct

Baadhi ya mambo yaliyoongezwa katika Instagram.

Uwezo wa kusambaza na kupokea picha mlalo ama Landscape.

Picha katika instagram direct kwa muda mrefu zimekuwa ni zile ambazo zipo katika umbo la kusimama ama portrait jambo ambalo lilileta shida pindi mtu anapotaka kusambaza picha katika umbo mlalo. Pia video kabla ya maboresho haya zilikuwa zinatumwa katika umbo mraba lakini sasa watumiaji wataweza kutuma video katika ombo halisia la video husika.

INAYOHUSIANA  Mambo yanayokera katika makundi ya WhatsApp

Mengine yaliyokuja na maboresho haya.

Uwezo wa kupiga namba za simu kutokea katika instagram direct moja kwa moja ni jambo jingine ambalo limeongezwa katika mtandao huu, kwa sasa namba zote za simu na anuani zitakuwa zinapewa kiunganishi kwaajiri ya kufanya majukumu mengine ambayo hayamo katika instagram kama vile kupiga simu na kutuma ujumbe.

Endelea kufuatilia mtandao wako wa Teknokona kwa habari motomoto za Teknolojia, pia tufuate katika mitandao ya jamiii kama Facebook Twitter na Instagram.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.