Maboresho: Twitter yazidi kuwabana wenye Matusi na Chuki

0
Sambaza

Mtandao wa Twitter umezidi kufanya jitihada za kuondoa ukandamizaji chuki na matusi katika mtandao huo ili kuongeza watumiaji hai wa kila siku.

Meneja wa bidhaa wa kampuni hiyo amethibitisha katika bandiko lake katika blogu kwamba kampuni hiyo italeta huduma mbili kusaidia kuifanya  jukwaa hilo kuwa rafiki zaidi.

twitter_12

Huduma hizo mpya za Twitter zinalenga katika kupunguza kama sio kuondoa kabisa chuki matusi na ukandamizaji, mambo haya yamekuwa ni kama kikwazo kwa wengi hasa watu maarufu ambao wamekuwa wakiandamwa kwa matusi na chuki.

SOMA PIA:  Uwezo wa kumuongeza mtu kwenye kundi la WhatsApp bila Admin kujua

Notifications kutoka kwa watu unaowafuata tu!

Kwa sasa watumiaji wa Twitter wataweza kuchuja notifications zinazokuja katika mtandao huu kwa kufanya kwamba wasijulishwe pindi mtu ambaye hawamfuati anapojibu ama anapokuandikia bandiko, hii inamaana kwamba watumiaji wa Twitter watakao chagua kutumia huduma hii watataarifiwa pale tu watu ambao wamewachagua wao watakapo jibu ama kuwaandikia bandiko.

Quality Filter

Kipengele hiki kitasaidia kuchagua mabandiko ambayo utayaona katika timeline yako, ingawa haita ficha mabandiko kutoka kwa watu ambao unawafuata lakini itaondoa tweets zote ambazo zinaonekana zinajirudia ama zimetumwa na mashine.

chuki

Picha ikionesha maelekezo ya jinsi ya kuanzisha huduma hiyo mpya.

Twitter ipo katika vita ya muda mrefu ya kujaribu kuendelea kupata watumiaji wengi zaidi, hivyo ni wazi jitihada hizi ni moja kati ya hatua zake za kujaribu kulifanya jukwaa hili mahali salama kwa kila mtu hivyo kuongeza watumiaji.

SOMA PIA:  Huduma ya WhatsApp ilivyopotea jana usiku katika mataifa mengi

Katika habari nyingine mtandao huu pia leo umetangaza kwamba umezifunga akaunti zipatazo 235000 zikituhumiwa kusambaza chuki na kuhamasisha ugaidi jambo hili linaiweka Twitter katika mstari wa mbele katika mapambano zidi ya ugaidi ukifananisha na mitandao mingine.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com