Maboresho: WhatsApp kuleta Albamu na meseji za kufutika.

0
Sambaza

WhatsApp imeendelea kuonesha dhamira yake ya kubakia kuwa mtandao mkubwa zaidi katika mitandao ya kijamii, hili linadhihirika baada ya mtandao huo ambao unamilikiwa na Facebook kufanya majaribio ya Albamu za picha, filters na pia meseji za kufutika.

WhatsApp kuleta Albamu

WhatsApp kuleta Albamu: Muonekano wa toleo jipya la Whatsapp lenye mabadiriko.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za teknolojia Techcrunch, toleo jipya la mtando huu linategemewa kuleta mambo mapya matatu kama ifuatavyo-:

SOMA PIA:  Google yaongeza lugha ya kiswahili katika voice search

Albamu za picha katika gumzo.

Toleo jipya linalokuja linasemwa kwamba picha zaidi ya moja ambazo zinatumwa katika gumzo zitaunganishwa katika albamu moja ya picha, hii inategemewa kuondoa kero ya picha nyingi kuchukua nafasi ya sehemu ya gumzo.

WhatsApp kuleta Albamu

WhatsApp kuleta Albamu

Filter za picha.

Imekuwa shida kwa muda mrefu kwa wapenda filters pale inapokuja app ya WhatsApp maana haikuwa na uwezo wa kurekebisha picha unazopiga ndani ya app hii. Kwa sasa watumiaji wataweza kuchagua kati ya filter tano ambazo zipo kwaajiri ya picha utakazo piga ndani ya app hii.

Muonekano wa filter katika picha ndani ya WhatsApp

Meseji za kufutika.

Inasemekana kwamba Whatsapp wanataka kuleta uwezo wa mtu kufuta meseji picha gif ama video ambayo tayari umeishatuma, pengine hii ni moja kati ya vitu vya muhimu sana vilikuwa vinakosekana katika mtandao huu ( kumbuka msg mbali mbali unazokosea kutuma katika makundi).

SOMA PIA:  Airtel Care - App inayorahisisha huduma mbalimbali kwa wateja wa Airtel

Baada ya kupakua toleo jipya la Whatsapp na kulijaribu tumegundua kwamba huduma hii bado haijaachiwa lakini ni mategemeo yetu kwamba inakuja siku za usoni.

Njia fupi ya kujibu ujumbe katika gumzo.

Mpaka sasa kama unataka kujibu meseji fulani katika mazungumzo ya WhatsApp inakubidi kubonyeza huo ujumbe kwa muda mpaka utakapopata menyu ambapo utachagua kujibu ujumbe, jambo hilo huchukua muda mrefu kidogo na pengine ndio maana wameleta njia fupi. Kwa sasa kujibu ujumbe utaswap tu katika ujumbe unaotaka kuujibu katika mazungumzo ama gumzo.

SOMA PIA:  Uber yaboresha huduma zake kuvutia zaidi katika msimu wa sikukuu

Kama tayari toleo hili jipya limekwisha kukufikia tuambie nini maoni yako juu ya maboresho hayo!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com