Mac Pro iliyoboreshwa na yenye nguvu zaidi kutoka Apple

0
Sambaza

Mwaka 2013 Apple walilteta sokoni kompyuta zilizotekea kupendwa na wengi kutokana na uwezo zilizokuwanazo na kuonekana kuwa kompyuta zenye nguvu zaidi lakini tangu mwaka huo Apple hawajatoa toleo jingine la Mac Pro.

Mwezi Aprili 2017 kampuni iliyojikita zaidi katika utengenezaji wa vifaa vya kieletroniki kama simu na kompyuta ijulikanayo kama Apple imeweka wazi kuwa toleo jipya la Mac Pro lipo njiani kutoka na watu wasidhani kuwa hakuna matoleo mengine ya Mac Pro.

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kuruhusu uso mmoja tu kusajiliwa

Apple imethibitisha kuwa jopo la watu linafanyia kazi muundo wa toleo jipya la Mac Pro ambao utakuwa na maboresho mengi. Mac Pro haikuwahi kuwafinyiwa maboresho tangu itoke mwaka 2013.

airtel tanzania bando

Sifa za toleo jipya la Mac Pro

Aina mbili tofauti za Mac Pro zina sifa zifuatazo:-

  • Ya kwanza itakuwa na CPU sita za Xeon na kwa upande wa ubora wa picha ikiwa na dual AMD G500 GPUs huku zikiuzwa dola 2,900|zaidi ya Tsh. 6,670,000.

    Toleo jipya la Mac Pro linategemewa kuingia sokoni mapema mwakani, kwa mwaka huu Apple wanatarijia kuleta Pro Display.

  • Ya pili itakuwa na prosesa 8 na kwa upande wa kufanya picha zionekane zenye ubora wa juu inatumia dual D800 GPUs. Itauzwa kwa $3,900|zaidi ya Tsh. 8,970,000.
SOMA PIA:  Namna ya kubadili folda lako kuwa la rangi uitakayo katika Windows! #Maujanja

Apple ambao kila mara wanalta matoleo ya vifaa vyao mbalimbali mwaka huu wanatajia kutoa toleo jipya la iMac iliyoboresha na nyenye nguvu zaidi. Kama wewe ni mpenzi wa iMac basi jiandae kifedha ili uweze kununua toleo jipya la iMac.

Vyanzo: The guardian, CNBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com