Machi 19 Pope Francis Atajiunga na Instagram, Ingia Kujua Zaidi!

0
Sambaza

Kwa sasa Pope Francis amejiweka tofauti na ma Pope wengine waliopita juu ya vitu vingi sana. Kwa mfano katoa sauti yake juu ya mambo mengi sana kama ndoa za jinsia moja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pope Francis pia inasemekana kuwa anataka kuweka rekodi ya kuwa Pope ambaye anapenda teknolojia kwa kuongezea katika akaunti yake ya Twitter amesema kuwa ataweza kuingia kwa mara ya kwanza katika mtandao wa kijamii unaohusisha picha na video yaani Instagram.

Pop Francis Akiwa Na Tim Cook Wa Apple Inc.

Pop Francis Akiwa Na Tim Cook Wa Apple Inc.

Kutokana na ripoti zilizopo ni kwamba akaunti hiyo itafunguliwa ifikapo machi 19 mwaka huu. Ripoti inaongezea  kuwa Pope Francis atatumia jina la buy me a rose lyrics @Franciscus katika mtandao huo wa Instagram.

INAYOHUSIANA  Waanzilishi wa Instagram waacha kazi

Pope Francis ambaye kwa kipindi cha mda mrefu amekuwa akisifu uwezo wa intaneti katika kukuza na kujenga jamii bora ambayo iko radhi ku’share’ mambo mbalimbali baina ya watu wake, amekuwa katika makutano ya siri na  bwana Kevin Systrom, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Instagram mwezi uliopita.

Hakuna ushahidi ambao unainyesha kuwa Bw. Kevin Systrom alimwalika Pope ilimradi tuu kutengeneza akaunti yake ya instagram. Lakini kutoka kwa akaunti ya Kevin ndani ya Instagram, waliongelea juu ya jinsi gani picha inaweza ikawa na uwezo mkubwa katika kuwaleta watu karibu duniani kote bila ya kujali mipaka kama vile lugha na tamaduni.

INAYOHUSIANA  Muda chache kwenye mitandao unapunguza upweke

Ukiachana na utakatifu wake mwingi alionao bado Pope ana Followers Milioni 8.88 katika mtandao wake wa Twitter ambapo anatumia jina la @Pontifex ambapo alijiunga mwaka 2012. Na hapo bado ana akaunti zingine 8 ambazo ni ‘Official’ na zinatumia lugha tofauti tofauti zikijumuisha kitaliano, kifaransa na kiarabu.

Pope licha ya upendo wake katika Teknolojia pia ameshauri kuwa watu wasiwe wanatumia vifaa vyao wakati wa kula chakula. Na pia familia ambazo haziongei na kula pamoja ( katika Meza moja) hazihesabiki kama ni familia.

Kwa hamu kabisa, naisubiria akaunti hii ya where to buy aciclovir @Franciscus katika mtandao wa Instagram. Jambo nnalolisubiria ni kuona picha ya kwanza ya pope katika akaunti hiyo na ndani ya siku moja itakuwa na followers wangapi – Kaa na mimi mkao wa kula – Zaidi tembelea TeknoKona kila siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.