Magari zaidi ya Milioni 100 kutoka Volkswagen Hatarini Kudukuliwa na Kuibiwa

0
Sambaza

Magari yasiyotumia funguo (keyless remote) kutoka kampuni ya Volkswagen yapo katika hatari kubwa ya kudukuliwa mfumo wake wa kufunga(lock) na kuwasha gari.

Teknolojia inavyozidi kukua na ndivyo ambapo vitu vingine tunavyovitumia kila siku kama vile magari n.k navyo vinaboreshwa zaidi.

volkswagen hatarini

Magari zaidi ya Milioni 100 ya Volkswagen hatarini kudukuliwa

Lakini kwenye teknolojia na usalama kuna imani moja kuu ambayo ni kwamba kila unavyozidi kuboresha programu flani basi na ndivyo kazi ya kuhakikisha inakuwa salama kutoka kwa wadukuzi inavyozidi kuwa kubwa na ngumu.

orlistat order online canada Kundi la watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham wamechapisha taarifa inayoonesha waliweza kudukua rimoti za magari ya VW (Volkswagen) kwa kuwa eneo la karibu na mtu anaye bonyeza rimoti yake kwa ajili ya kufunga (lock) au kufungua (unlock) gari lake.

Wadukuzi wakiweka mitambo yao karibu na mtu anayeondoa au kuweka ‘lock’ ya gari lake basi wao wataweza kutengeneza nakala nyingine ya funguo kama hiyo

Inasemekana mtu aliyepanga kudukua na kutengeneza nakala nyingine ya rimoti za gari flani ataitaji tuu kuwa na eneo la karibu na kuweza kuingilia mawasiliano ya rimoti halisi na gari pale mtu anapolock au kuondoa lock.

INAYOHUSIANA  Fahamu kama simu zako zinafuatiliwa

Namba ya magari yanayoweza kuathirika ni mengi sana (milioni 100) kwa kuwa mfumo huo umetumika kwenye magari mengi sana kuanzia mwaka 1995 (familia yaani ‘Models’ za Audi, VW, Seat na Skoda).

Volkswagen wamesemaje?

Msemaji wa kampuni ya VW ameonekana kukubali matokeo ya watafiti hao kwani alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo alisema matoleo yao ya magari ya sasa hayaathiriki na udukuzi huo akionekana kuepuka kuongelea yanayoathirika.

Je ni vigumu sana kudukua?

Inasemekana upatikanaji wa bei rahisi wa vifaa mbalimbali vya teknolojia ya kimawasaliano ya redio unarahisisha sana mtu yeyote mwenye ujuzi na nia ya kufanya udukuzi na uibaji wa magari hayo kufanikiwa.

INAYOHUSIANA  Dar nzima kufungwa kamera za CCTV

http://signaturemassagekcmo.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://signaturemassagekcmo.com/therapeutic-cupping-therapy/ Soma Pia 

Uwezekano wa nywila yako Kujulikana kama unatumia Wireless Keyboard

Hacker ahukumiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kudukua siri za Jeshi la Marekani

Ingawa ukuaji wa teknolojia unakuja na faida zake ila pia inaonekana changamoto zinazokuja pamoja na teknolojia za kisasa zinazidi kukua na hasa hasa kwenye masuala ya usalama dhidi ya udukuzi (hacking).

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.