Magari yanayojiendesha yenyewe kutoka Google yana uwezo wa kulihisi gari la polisi

0
Sambaza

Katika nia ya kujiimarisha katika biashara ya magari yanayojiendesha yenyewe Google wanaweka sensors kwenye magari hayo ili kuweza kuhisi gari la polisi.

Magari hayo yanafanyiwa maboresho na kuwa na sensors ambazo kazi yake itakuwa ni kuweza kuhisi gari la polisi ambalo litakuwa katika eneo hilo.

Teknolojia hiyo itawezesha magari yanayojiendesha yenyewe kutoka Google kuweza kulitambua gari la polisi pamoja na rangi ya taa ambayo itawashwa na kupiga king’ora na gari hilo la Google kukaa pembeni (itakapobidi) na kusubiri kuulizwa maswali na polisi.

Polisi akifanya kazi yake bada ya kulisimamisha gari linalojiendesha lenyewe kutoka Googke.

Polisi akifanya kazi yake bada ya kulisimamisha gari linalojiendesha lenyewe kutoka Google.

Sababu ya Google kufanyia maboresho magari yao yanayojiendesha yenyewe

Sababu kubwa ni kuvutia wateja na kuzidi kupata faida kutokana na magari hayo na kujiweka vizuri kakika soko la ushindani ambalo kwa hakika magari yanayojiendesha vizuri yametokea kupendwa na wengi.

SOMA PIA:  Tecno Wazindua Simu Mpya Ya Phantom 8!

Faida za maboresho katika magari hayo

Kwa hakika sasa Google hawatakuwa na wasiwasi kuweza kutambua gari ya polisi kwani hivi sasa magari hayo yamewekwa ‘sensors’ zinazoyawezesha kuweza kuyatambua magari ya polisi yakiwa yanasogelea gari husika.

Gari linalojiendesha lenyewe kutoka Google linaloweza kuhisi gari ya polisi linapokuja.

Gari linalojiendesha lenyewe kutoka Google linaloweza kuhisi gari ya polisi linapokuja.

Kwa sheria za Magharibi hususani Uingereza dereva anatakiwa kusimama kituo sehemu ambayo ni salama baada ya kupewa ishara ya kusimamisha gari na polisi anaweza akasimamisha gari kwa sababu yoyote tu.

SOMA PIA:  Hukumu ya Mahakama: Simu ya mkononi imesababisha uvimbe katika ubongo wa mtumiaji

Tembelea tovuti yetu kila leo kuweza kuhabarika kwa lugha yako adhimu ya Kiswahili. TeknoKona kwa maunja mbalimabli na kiteknolojia zaidi.

Vyanzo: Telegraph, Siliconbeat

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com