Majaribio ya makazi ya kujazwa upepo ktk anga yafanikiwa! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Majaribio ya makazi ya kujazwa upepo ktk anga yafanikiwa! #Teknolojia

0
Sambaza

Baada ya kushindwa kufanikisha jaribio la makazi ya kujazwa upepo kwa kujaza upepo chumba cha mfano wa makazi hayo wiki iliyopita NASA hatimaye mwishoni mwa wiki ilifanikiwa kujaza upepo kichumba hicho ambacho kinatumiwa kwa majaribio.

source url

Ingawa jaribio hili limefanikiwa na kichumba hicho kika jazwa upepo na kujaa bado itabidi tusubiri mpaka wiki moja ndipo mwanaanga atakwenda na kujaribu kuingia katika chumba hicho.

go site

Muonekano wa kisanii ukionesha jinsi gani mfumo huo wa makazi ungeonekana baada ya kuunganishwa kwenye kituo cha anga cha kimataifa

http://jarviscre.com/about/ Muonekano wa kisanii ukionesha jinsi gani mfumo huo wa makazi ungeonekana baada ya kuunganishwa kwenye kituo cha anga cha kimataifa

Wiki iliyopita NASA ilisitisha zoezi hili baada ya zoezi la kujaza upepo kufanyika kwa muda mrefu bila ya kuonesha mafanikio katika uongezekaji wa ukubwa wa chumba, awali ilitegemewa kwamba baada ya zoezi la kujaza upepo kufanyika kwa muda mfupi na chumba hicho kidogo kilichounganishwa katika kituo cha kimataifa cha anga kingeongezeka ujazo na ukubwa lakini hili halikutokea katika majaribio hayo hali iliyopelekea misheni hiyo kusitishwa ili wahandisi wa NASA na Bigelow (ambao ndiyo waliobuni makazi hayo ya kujazwa upepo) wakae na kutafuta chanzo cha tatizo hilo.

makazi ya kujazwa upepo

makazi ya kujazwa upepo: Muonekano wakati wa hatua za mwanzo za kutanua makazi hayo.

Baada ya uchunguzi wataalamu hao kutoka NASA na Bigelow waligundua kwamba vitu vilivyotumika kutengeneza makazi hayo ya kujazwa na upepo hubadili tabia zake pindi vinapokuwa katika anga hasa kama vilikuwa vimekandamizwa saana.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Wataalamu hawa wamekuja na kauli moja kwamba katika hatua za kuutoa mzigo huu duniani kwenda katika kituo cha anga cha kimataifa mzigo huu ulikandamizwa saana kwa muda mrefu kitu ambacho kilipelekea material ya nayotumika kutengeneza makazi hayo kubadilisha tabia zake katika anga kwa muda fulani ambalo ndilo jambo ambalo liliyazuia kuweza kutanuka kama yalivyotarajiwa na jambo hili sio la kudumu ila ni kwamba baada ya muda katika anga material haya hurudi katika hali yake ya kawaida.

makazi ya kujazwa upepo

Makazi ya kujazwa upepo: Mchoro kuonesha muonekano wa ndani wa makazi haya

Kwa ufupi ni kwamba Mzigo wa makazi haya ambao ulisafirishwa na Space X kwenda katika kituo cha anga ulikuwa umekandamizwa kwa muda hivyo ulipofika angani material haya yalibadilika tabia na kuwa yanachelewa kutanuka na hili hasa ndio lilikuwa chanzo cha kushindwa kwa jaribio la kwanza, baada ya kukaa kwa muda material haya yakarudia tabia yake ya kawaida ndio maana baada ya kufanya zoezi hilo kwa mara ya pili zoezi mafanikio yakapatikana.

INAYOHUSIANA  Sababu 5 kwanini ndege inapata ajali

Baada ya kujaza kichumba hicho upepo na kichumba kutanuka kama ilivyo kusudiwa kitaangaliwa kwa karibu wiki moja kabla ya mwananga wa kwanza hajaingia na kukijaribu.

Vyanzo: mitandao mbalimbali ambayo iliripoti habari hii kama vile Engadget

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.