Makaburi matatu yawekwa Wi-Fi jijini Moscow Urusi

0
Sambaza

Makaburi matatu yanayotembelewa sana na watu jijini Moscow yawekewa huduma ya intaneti/mtandao ya wi-fi. BUREEEE

Makaburi hayo yanayotembelewa sana, wanaotembelea wataweza kutumia mtandao wa intaneti bila malipo katika makaburi ya Novodevichy, Troyekurovskoye na Vagankovo  na huduma hiyo ilianza mapema mwaka huu kwa mujibu wa tovuti ya Moscow City.

Makaburi matatu yawekwa Wi-Fi

Makaburi matatu yawekwa Wi-Fi : Aliyekuwa mwandishi mashuhuri wa nchini humo, Anton Chekhov ni mmoja wa watu mashuhuri waliozikwa Novodevichy

 

Mkuu wa huduma za makaburi mjini Moscow Bw. Artem Yekimov anasema lengo ni kusaidia wageni kwenye makaburi hayo kutafuta habari zaidi kuhusu watu mashuhuri waliozikwa humo. Aidha, kuwafanya wafurahie matembezi yao makaburini.

SOMA PIA:  Hatimaye kampuni ya Verizon yainunua Yahoo!

Kampuni ya mawasiliano ya “YS System” inasema ilijitolea kuweka huduma ya wi-fi humo baada ya kusikia mipango ya kutenga maeneo ya watu “kutulia kisaikolojia” katika makaburi hayo.

Makaburi ya Novodevichy ni moja ya maeneo yanayotembelewa sana na watalii Moscow. Miongoni mwa watu waliozikwa humo ni mwandishi Anton Chekhov, kiongozi wa zamani wa muungano wa Usovieti (USSR) Nikita Khrushchev na rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin.

Soma Pia – Makanisa Kuwekwa WiFi nchini Ujerumani

SOMA PIA:  Simu janja 6 za Xiaomi kutopata masasisho tena

Je unalionaje jambo hili? Ni sawa au?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com