Makampuni makubwa ya simu duniani: Huawei waikaba Apple katika nafasi ya pili

0
Sambaza

Kampuni ya Huawei imezidi kukua na sasa inatishia kuipokonya Apple nafasi ya pili katika orodha ya makampuni yanayoingiza sokoni simu nyingi zaidi.

Kwa muda mrefu sasa nafasi ya kwanza imekuwa ikishikiliwa na Samsung, kufuatiwa na Apple na Huawei imekuwa inashika nafasi ya tatu. Ila uporomokaji wa mauzo ya simu za iPhone imeifanya Apple kupunguza idadi ya simu inazotengeneza ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2015.

Huawei wanamiaka chini ya 5 katika biashara ya utengenezaji simu…na tayari wamewaacha mbali Sony, HTC na LG – makampuni ambayo yalikuwa juu zaidi yao katika biashara hiyo. Ndani ya miezi 12 kuna uwezekano mkubwa Huawei wakaipokonya Apple nafasi ya pili.

huawei makampuni makubwa ya simu

Makampuni Makubwa ya Simu Duniani: Muoneakano wa idadi ya simu zinazoingizwa sokoni kutoka kwa makampuni makubwa 3 ya juu zaidi. (Muda: Robo mwaka, 2015 -2016

Ni siku chache tuu zilizopita tayari Huawei wametambulisha simu janja ya kiwango cha juu cha ubora na inaonekana simu hiyo, Huawei Mate 9, itaweza nufaika kutokana na majanga ya Samsung Galaxy Note 7 na hivyo kuuzika vizuri zaidi. Simu hii ya Huawei ikifanya vizuri sokoni basi kuna uwezekano mkubwa sana miezi michache ijayo Huawei watanyakua nafasi ya pili kutoka Apple kwani tayari wamewabana kwelikweli.

Kutokuwepo kwa simu za Galaxy Note 7 sokoni kunamaanisha simu yao mpya ya Huawei Mate 9 haitapata ushindani mkubwa sokoni kwenye simu za ukubwa wa inchi 5.5 na zaidi..

Simu Huawei Mate 9 Porsche

Muonekano wa simu ya Huawei Mate 9 toleo la Porsche na toleo la kawaida.

Na pia ingawa kwa muda mrefu Huawei wamekuwa wanatumia kiasi kidogo cha pesa kwenye matangazo (marketing & advertising) kwa kipindi hichi wamezidi kuongeza bajeti katika eneo hilo.

Lionel Messi Akionyesha Saa Yake Mpya Ya Huawei

Lionel Messi Akionyesha Saa Yake Mpya Ya Huawei

Mjumlisho wa utumiaji wa pesa nyingi zaidi kwenye kujitangaza pamoja na uletwaji wa simu janja za kiwango cha juu zinazokubalika katika masoko ya Ulaya na Marekani kunaiweka Huawei katika nafasi nzuri zaidi kimafanikio kimauzo.

Je una mtazamo gani juu ya simu za Huawei na mafanikio yake?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com