Majaribio ya makazi ya kujazwa upepo katika anga yakwama!

0
Sambaza

NASA leo imekutana na kigingi katika majaribio yake ya makazi ya kujazwa upepo katika kituo cha anga cha kimataifa ISS, makazi haya ambayo yalisafirishwa na roketi ya Space X kufika katika kituo hicho cha anga (na roketi hiyo ilitua duniani bila kuharibika). Hili ni pigo kubwa kwa wadau wa sayansi ya anga ambao walikuwa wanalifuatila tukio hili kwa karibu.

makazi ya kujazwa upepo

Muonekano wa kisanii ukionesha jinsi gani mfumo huo wa makazi ungeonekana baada ya kuunganishwa kwenye kituo cha anga cha kimataifa

Kwanini wanaanga wanataka kutumia makazi ya kujazwa upepo?

Moja ya lengo la wanaanga ni kuhakikisha kwamba binadamu wanaweza kwenda kutaliii ama kuishi katika anga ama sayari nyingine, changamoto ni jinsi ya kutengeneza makazi ya watu watakao kwenda angani ama katika sayari nyingine.

SOMA PIA:  Ndege za bila ya rubani/drones kusimamiwa zaidi Uingereza

Njia pekee ni kusafirisha makazi haya kwa kutumia roketi zinazoenda angani lakini njia hii inakumbana na changamoto kwamba kusafirisha makazi ni gharama hivyo ikapelekea kuzaliwa kwa wazo la kutumia makazi ambayo yanakunjwa katika ukubwa mdogo kisha yakifika angani ama katika sayari yanakunjuliwa kisha kujazwa upepo.

Soma pia

Kituo cha kuongoza misheni za kituo hicho cha anga cha kimataifa kilimuamuru mwanaanga Jeffrey Williams kusitisha zoezi hilo baada ya masaa mawili kupita bila ya mafanikio wakati ilitegemewa kwamba zoezi lingetumia muda mfupi. Kituo cha kuongoza kili mjulisha mwanaanga huyo kusitisha zoezi hilo ili wahandisi waangalie ni kwanini halikufanikiwa.

SOMA PIA:  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Makazi haya ya kujazwa upepo yalibuniwa na kutengenezwa na kampuni inayoitwa Bigelow ambayo ililipwa na NASA kutengeneza na kuyafanyia majaribio makazi hayo. Makazi haya  yalisafirishwa kwenda katika kituo cha kimataifa kwa kutumia roketi ya Space X ambayo ili fanikiwa kupeleka mzigo angani na kisha kurudi na kutua salama (kitu ambacho siku za nyuma kilikuwa hakiwezekani.)

Kushindwa huku kwa jaribio hakuna maana kwamba mpango wa matumizi ya makazi yanayojifungua angani umeishia hapa, hii ni changamoto tu ambayo watu wengi wanaamini kwamba itatatuliwa na zoezi litakamilika kama ilivyokuwa imepangwa awali.

SOMA PIA:  Huawei Wazalisha Simu Chache Zenye Chata La KFC Huko China!

Je wewe ni shabiki wa habari za sayansi ya anga? kama jibu ni ndio hizi ni makala nyingine nilizoziandika kuhusu sayansi ya anga.

Soma pia

VYANZO; makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao wa Space

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com