Malori yajiendeshayo yenyewe yakamilisha safari Ulaya

0
Sambaza

Msafara wa malori yajiendeshayo yenyewe (kwa kiasi kikubwa) yamekamilisha safari katika mji wa bandari wa Rotterdam nchini Uholanzi, hii ni safari ya kwanza ya magari kama hayaa kuweza kuvuka mpaka wa nchi  yakitokea nchi za Sweden na pia kusini mwa Ujerumani.

malori yajiendeshayo yenyewe

Malori haya yanatoka katika kampuni za untengenezaji wa malori ambayo kwa pamoja zinatengeneza kundi la malori ambayo yanasafiri pamoja, tukio hili linaitwa platooning challenge na linahusisha malori yajiendeshayo yenyewe kwa kupokea taarifa juu ya kuongeza mwendo ama kupunguza mwendo kutoka katika gari lililombele kabisa.

SOMA PIA:  HP yatoa printer ndogo inayoenea kwenye kiganja cha mkono #Teknolojia

Tofauti ya magari haya na magari yajiendeshayo kama yale ya Google ni kwamba malori haya yanakuwa na gari moja ambalo limetangulia na linaendeshwa na binadamu na lori hili lililo mbele linatuma taarifa kuhusu breki na kuongeza mwendo  kwa kutumia njia ya Wi-Fi kwenda gari la nyuma.

Waandaji wa shughuri hii nzima wanasema kwamba kufanikiwa kwa safari hii kunamaana kubwa hasa kwa sekta ya usafirishaji wa mizigo katika bara hilo la ulaya. Inasemekana kwamba kwa kuwa ajari nyingi zinatokana na makosa ya binadamu basi malori yajiendeshayo yenyewe yatasaidia kupunguza ajari kaitka barabara za bara hilo.

SOMA PIA:  Baada ya Huawei Mate 10 kutoka sasa ni zamu ya Huawei Mate 10 Pro

Tafiti zinaonesha kwamba matumizi ya mafuta yanapungua iwapo Malori yatatumia mfumo uliotumiwa na malori hayo, pamoja na hilo pia imegundulika kwamba njia hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa foleni za magari.

Njia hii inahusisha magari mawili ama matatu ambayo yanakuwa yanalifuata gari moja ambalo ndilo linalotoa taarifa zinazotumika kuendesha mengine ambayo yanafuata.

Teknokona inaendelea kukuletea taarifa mbalimbali kuhusu teknolojia katika lugha yako ya kiswahili, endelea kutufuatilia katika mitandao ya kijamii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com