Mambo 5 Yaliyobadilishwa na Teknolojia – Fahamu kama unavyoelewa ni sahii au si sahihi!

0
Sambaza

Teknolojia inakua sana! Kwa teknolojia ambayo inakua kwa kasi kiasi hiki taarifa ya jinsi gani ya kuitumia ipasavyo inaweza ikaja na kuondoka haraka pia. Njia sahihi ya ufanyaji kazi ya jana inaweza ikawa ya kimakosa kesho.  Na ushauri mzuri wa kuepukana na balaa unaweza ukawa sio tena.

Leo tutangalia baadhi ya teknolojia ili kujua – Je, ni sawa inabidi zitumike kama tunavyojua au la hasha. Hii itajumuisha kuanzia teknolojia ya betri na zingine kadha wa kadha

1. Usichaji Kifaa Chako Usiku Kucha

Watu wengi wanafikiri si vizuri kuchaji vifaa vyao uskiku kucha wakati wamelala. Wanachoogopa ni kwamba wanafikiri vifaa hivyo vitajaa chaji sana na kulipuka au wanaweza wakaharibu betri za vifaa hivyo.

Acha uwoga! Hakuna tatizo kabisa unaweza ukachaji kufaa chako usiku kucha. Kumbuka teknolojia ya siku hizi inawezesha vifaa vyetu kutoingiza chaji tena pindi betri zimejaa kabisa. Kitu cha muhimu cha kuzingatia, inabidi kifaa hicho kiwe sehemu ambayo kinaweza kupata hewa ya kutosha – usiweke chini ya mto – kama bado unakipenda kifaa chako na kujipenda mwenyewe 🙂 .

2. Usitumie Chaja  Za Makampuni Mengine

Kuna watu wanaamini kuwa ukibadilisha Chaja na kutumia ya kampuni nyingine basi simu yako inaweza ikafa. Kwa mfano kuna watu wanaamini kama una simu ya Samsung basi inakubidi utumie chaja orijino ya Samsung tuu.

SOMA PIA:  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

Kumbuka kuna ina mbili za chaja kutoka kwa makampuni mengine ya kwanza ni zile chaji ambazo zinaweza kuchaji kifaa chako kwa spindi ndogo sana yaani simu inachukua muda mrefu ili kujaa. Chaja aina ya pili ni zile sasa unazosikia stori za kutishatisha juu yake. Chaja hizi mara nyingi zinakuwa hazina jina, au zinaweza zikasema zinatoka katika makampuni kama Apple, HTC, Samsung N.k lakini zinakuwa  na bei ndogo ajabu.

Chaja hizi ndio zile unazosikia zinavimbisha betri au zinafanya liungue kabisa. Cha muhimu kujua ni kwamba zile chaja ambazo zinachaji kwa taratibu ni sawa tuu kuzitumia. Lakini ili kuwa katika upande salama inabidi ukanunue chaja sehemu ambayo inafahamika inauza vitu orijino – vyenye ubora. Epuka chaja za bei rahisi ili ili mradi tu uwe na chaja – ni hatari!

3. Huwezi Ukafuta Taarifa Mara Moja, Moja Kwa Moja Katika Kompyuta

Natumai unajua kwamba ukifuta faili katika kompyuta halifutiki moja kwa moja. Faili hilo linakuwa bado linaelea sehemu katika ‘Hard Drive’ yako na kusubiria ile sehemu ichukuliwe na faili lingine. Mpaka jambo hili litekelezeke unaweza ukawa umeshalipata faili lako (tena)

Kama unauza au unagawa kompyuta yako inabidi kuwa na uhakika kabisa kuwa mafaili yako yamefutika kwa sababu utakuwa hujui ni kiasi gani cha taarifa mtu anaweza kupata kutoka katika mfumo wa kompyuta hiyo.  Sasa Utahakikishaje hakuna kilichobakia??

SOMA PIA:  CCleaner: Programu muhimu ya kusafisha kompyuta iliyogeuka kuwa kirusi

Njia ya haraka haraka hapa ni kujaribu kutumia program zile maalum za kukuwezesha kufuta vitu. Programu hizi zinakuwa zinafanya kazi kwa ufanisi kuliko ukiamua kufuta taarifa zako kwa njia ya kawaida. Lakini ukiangalia kwa jicho lingine unaweza kufanya haya yafuatayo

  • Acha vifaa vyako nyumbani na kuvitumia kwa kazi zingine
  • Unaweza pia ukaondoa ‘Hard drive’ katika kompyuta yako, kabla ya kuigawa na kuihifadhi, kuigeuza kuwa ‘external’ au ukaiharibu.

NYONGEZA: Katika nchi za watu ughaibuni, Serikali (police) wakitaka kuficha vitu vya siri vilivyo katika mfumo wa kielektroniki (kama hard drive). Cha kwanza kabisa wanafuta taarifa zote katika kifaa hicho kisha wanakiharibu kifaa hicho.

4. Kuperuzi Kwa Siri, Sio Kwa Siri Kama Unavyofikiria

Kila kivinjari kina kipengele cha kuperuzi kwa siri (private browsing). Ukiwa unaperuzi kwa siri katika mitandao kile kivinjari kitashindwa kurekodi  wapi unatembelea na pia kitakuwa kikiwa kinafuta taarifa nyingi amabazo pengine mtu ambae atakuwa anatumia kompyuta hiyo kutoweza kukuona.

Katika vivinjari vya Microsoft Edge, Internet Explorer, Firefox na Safari, unaweza ukaingia katika kuperuzi kwa siri kwa kubofya  CTRL + SHIFT + P (CTRL + OPTION + P katika Mac). katika Chrome, unatumia CTRL + SHIFT + N (OPTION + SHIFT + N katika Mac).

Kitu ambacho pengine huwezi kujua ni kwamba, kuperuzi kwa siri hakufichi taarifa zako za mtandao kwa watu wanaosambaza huduma ya intaneti, kama vile mtandao wako wa simu n.k. Kumbuka katika teknolojia kitu kikiwa cha siri (private) hiyo inamaanisha ni kigumu tuu kukipata. Kama unataka kuficha kabisa taarifa za mitandao unayotembelea basi tumia programu za VPN

SOMA PIA:  Samsung Galaxy X kuwa simu ya kwanza yenye kioo chenye kujikunja na kujikunjua? #Uchambuzi

5. Uwe Unazima Kompyuta Yako Kila Ifikapo Usiku

Ingekuwa hili limejitokeza zamani sawa kwa kiasi Fulani ningekubaliana na hili kwa kiasi, kwa sababu kwa kipindi hicho teknolojia ya kompyuta ilikuwa ya chini. Siku hizi kompyuta zimeboreshwa, inaweza kuhimili kutumika kwa muda mrefu. Ukiiacha usiku kucha hakuna tatizo. Kwa wale wanaopenda kudownload vitu usiku kucha ni sawa kufanya hivyo ila cha kuzingatia ni kwamba kompyuta iwe katika eneo la uwazi (iwe inapata hewa ya kutosha) na hakikisha kama ni kompyuta ya ‘desktop’ basi unatumia UPS kwa ajili ya kuhakikisha usalama pale umeme ukikatika na kurudi ghafla.

Ni njia gani kati ya hizo ulikuwa unaogopa kuzitumia kwa sana kwa kuhisi zinaweza zikaathiri kifaa chako? Tuandikie sehemu ya comment.

 Soma pia;

 🙂

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com