Facebook inapokua na taarifa zako nyingi hilo ni jambo zuri kwake kwa kua itaweza pata pesa kiurahisi kwa wanaofanya matangazo ambao wanataka kukufikia wewe ki urashisi. Mfano inaweza toa tangazo kwa watu wa Tanzania tuu kwa kuangalia nchi ulioijaza katika profile lako. Taarifa hizi ndogo ndogo zinaweza kukuletea matatizo
makubwa . sawa ni taarifa ndogo ndogo lakini ukizikusanya kwa ujumla? hapo ndipo mambo kama ‘Wizi Wa Utambulisho’ (Identity Theft) yanaweza jitokeza. Kwa bahati mbaya kuna mambo ambayo haipaswi kuyaweka wazi katika mitandao ya kijamii
Haya ndio mambo ambayo hutakiwi kayaacha wazi katika mitandao ya kijamii na jinsi ya kuzuia habari zako za muhimu endapo utakua huna njia mbadala isipokua kuziweka mtandaoni
1. Anwani Ya Nyumba Au Mahali Unapo ishi
karibia kila mtu ambae anaetaka kukuibia lazima ajue kwanza anuani ya nyumba yako. kuna mambo mengi yanaweza tokea juu ya swala hili. Mfano unaweza ukawa uko zako mahali pa starehe ukapiga picha kisha ukaisambaza katika mitandao ya kijamii (Facebook) wezi wakaona hii na wakajua kwa mda ule uko mbali na nyumbani wakachukulia hiyo kama sababu ya ziada kwa wao kuja kuiba katika nyumba yako kiurahisi. Kuwa makini kuwa hakuna taarifa kama hizo zinaonekana katika profile lako la facebook,
Ingia facebook bonyeza sehemu ya jina lako pale pembeni ya kiboksi cha ku ‘search’ ingia katika profile lako bonyeza ‘Update Info’ kisha katika upande wa “Contact and Basic Info” kuondoa anuani yako. Katika sehemu nyingine ambayo unaweza hisi taarifa za anuani yako hazitokei ni katika ‘Events’. taarifa zako zinatokea pale ili kuwa julisha wapi event hyo inafanyika . Hivyo basi futa event pale inapofanyika na pia waambie marafiki zako ambao wanahudhuria wakutumia meseji ili uwape taarifa za mahali inapofanyikia
2. Taarifa Za Mahusianio Yako Ya Kimapenzi
Kuweka wazi taarifa za mahusiano yako katika profile lako la facebook sio vizuri pia. Hata ukiachika kila mtu ataona pia namba za ‘likes’ utazopata unapotoka kwenye ‘dating’ (ndani ya mahusiano) hata ‘Married’ (Ndoa) kwenda ‘Single’ (Kuachika/kuacha) au ‘Its Complicated’ (Isiyo eleweka) zitaku shtua. Kulikua kuna App ya Facebook ambayo inakutaarifu kama rafiki yako katoka ndani ya mahusiano na kuwa ‘single’ hii inamaanisha taarifa zako zinasambaa kwa kiasi kikubwa
Ni rahisi sana kutoa taarifa za mahusiano yako kabisa mtandaoni na kuacha watu wajue katika makutano yao mengine na wewe
3. Taarifa Zako Za Malipo
Facebook ni ya bure, lakini bado inahitaji taarifa zako za kibenki kukuwezesha kununua vitu kadhaa kama vile ‘Gift cards’ na vingine vingi. Hatari inakuja pale unapoacha taarifa zako hizo facebook katika kompyuta ya nyumbani, ofisini au hata ya jamii. Ndugu wa karibu, rafiki au hata mtu asiye julikana anaweza kutumia pesa zilizopo kununua kitu, hutaki hilo litokee sio?
Na Pia hakuna uhakiaka kwa Facebook haitaweza shambuliwa siku moja na taarifa za muhimu kama hizo kuibiwa hivyo ni vyema kuwa makini
4. Namba Yako Ya Simu
Hii ni vigumu sana kuiepuka kwa kuwa sehemu za ‘Log in’ ‘Notification’ na nyinginezo nyingi zinatumia mara nyingi namba ya simu ya mtumiaji hata katika ku ‘sign up’ kuna baadhi ya watu wametumia namba zako za simu. Pia hata hivyo kama unatumia App ya Facebook katika simu yako itajua namba ya simu yako tuu. kwa mkono mwingine watu ambao una urafiki nao wataona namba ya simu yako hata kama hukutaka kuwapa.
kurekebisha hili, Ingia facebook bonyeza sehemu ya jina lako pale pembeni ya kiboksi cha ku ‘search’ ingia katika profile lako na bonyeza ‘Update Info’ kisha nenda katika sehemu ya “Contact and Basic Info” pembeni ya namba yako ya simu bonyeza ‘Edit’ kisha “Only Me.” na kisha click “Save Changes.”
5. Taarifa Zinazohusiana Na Kazi Yako
Hata taarifa za kazi yako si lazima zikae kwenye profile lako kama hazina faida ya kukaa pale. Taarifa hizo zinaweza sababisha mtu kukujua kwa urahisi kulingana na unapofanyia kazi, mtu anaweza kukufuatilia vitu unavyo ‘post’. Pia hata kama kuna wafanyakazi wenzio ambao hampatani atakua anakufuatilia ki urahisi na kuapata vile vitu ambavyo havitaki kutoka kwako kiurahisi. Na hata kama kuna watu wanataka kuvamia katika ofisi yenu wanaweza anza pata taarifa za hiyo ofisi kupitia taarifa katika profile lako.
Toa taarifa zozote zinazohusiana na kazi yako na kuwa mchaguaji juu ya wafanyakazi wenzio, wapi wanaweza kuwa ni marafiki zako facebook. Pia angalia status unazotuma je zinaendana nao na kazi yako?
No Comment! Be the first one.