Mambo nane binafsi ya kustaajabisha kuhusu Steve Jobs!

1

Sambaza

Steve Jobs alikuwa ni mtu tegemezi sana na daima atakumbukwa katika mchango wake kuhusiana na suala zima la teknolojia ndani na nje ya Apple (kampuni).

steve jobs

Bidhaa za Apple tangu kuanzishwa kwake zimekuwa zikipendwa na wengi jambo ambalo limeifanya Apple kama kampuni kupata faida kubwa kutokana na bidhaa zao na aliyekuwa mstari wa mbele kuanzisha utamaduni wa kuhakikisha Apple inatengeneza vitu vizuri alikuwa ni marehemu Steve Jobs.

Je, unajua kuna vitu alikuwa akifavifanya ambavyo vinaweza vikakuacha mdomo wazi?! Pata kuvijua vitu hivyo kama ifuatavyo:-

 1. Alikwa na ndugu aliyekuja kumfahamu ukubwani. Steve Jobs alikiwa na dada aitwaye Mona Simpon ambaye alikuja kumfahamu ukubwani katika miaka ya 90. Hii ilitokana na kwamba Steve Jobs alikuwa ni mtoto aliyeasiliwa (adopted) na wazazi wake hawakuwahi kumwambia kuwa alikuwa na dada. Mona Simpson ni mwandishi wa vitabu na katika kitabu chake ‘Anywhere but Here’ alizungumzia mahusiano yake (Mona) na wazazi wake. Jobs alikuja kujua ni dada yake baada ya kumfafuta.
 2. Baba mzazi wa Steve Jobs aliitwa  Abdulfattah JandaliWazazi wa Jobs walikuwa ni wahitimu katika chuo fulani ambao kwa upande fulani walikuwa hawataki mtoto kwa wakati huo ndio maana akaasiliwa. Sharti lao lilikuwa ni moja tu kwamba Jobs aasiliwe na wasomi wa chuo kikuu ambapo wazazi waliomuasili Jobs walidanganya kuwa ni wanakidhi kigezo hicho lakini wazazi halisi wa Jobs walikuja kugundua watu wale si wasomi wa ngazi ya chuo karibu wakatae kuruhusu mtoto wao aasiliwe na watu hao mpaka walihaidi kuwa wangehakikisha Jobs anafika chuo kikuu.
 3. Alitengeneza gemu iitwayo “Breakout”. Ndio, Steve Jobs alitengeneza gemu iliyojulikana kama Breakout. Ni gemu ambayo ilipokelewa vizuri na baadhi ya watu kuamini kuwa Steve Jobs ni moja ya watu 100 wenye akili nyingi sana.

  Gemu ya Breakout

  Gemu ya Breakout

 4. Alimkataa mtoto wake wa kwanza. Jobs alimkataa mtoto wake wa kwanza kwa sababu ya kuwa alikuwa hana uwezo wa kumpa mtu mimba. Sababu ya ukweli alikwa nayo mwenyewe moyoni lakini inawezekana ilikuwa damuni kwani hata yeye aliasiliwa. Lakini hapo baadae Steve Jobs alikubali na hata kuiita kompyuta aina ya “Apple III” Lisa (jina la mtoto wake wa kwanza).
 5. Pesa yake alikuwa haitumii kwa kutoa misaada (charity). Hii ilidhihirika pale alipokuwa CEO wa Apple kwani alziba mianya yote ambayo ilikuwa ikionyesha matumizi ya pesa kwa kutoa misaada na kusema mpka watakapopta faida ndio watakuwa wakitoa misaada. Jobs aliangalia sana katika utengenezaji wa vitu vya kiteknolojia vya kuiingizia Apple faida kubwa.
 6. Alimdanganya Steve Wozniak. Steve Wozniak ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa Apple alishirikiana na Jobs kutengeneza gemu ya Breakout ambapo mchongo mzima wa kutengeneza gemu hiyo Jobs alilipwa $5,000 lakini akamwambia kuwa amelipwa $700 tu. Ingia hapa kujua mengine kuhusu Steve Wozniak.

  Bw. Steve Wozniak

  Bw. Steve Wozniak

 7. Hakwenda chuo. Mark Zuckerberg na Bill Gates ni watu wanaojulikana kwa kutohitimu masomo yao chuo. Hivyo hivyo kwa Jobs nae hakuhitimu masomo yake  baada ya kujiunga na chuo cha Reed na kuacha baada ya muhula wa kwanza kumalizika.

 8. Alikula mboga aina ya samaki tu. Jobs alikuwa aakila samaki tu katika jamii ya mboga na kuwa tofauti na wanaokula mboga za majani tu (vegetarian) kwani wao wanakula maziwa na mayai. Watu wenye kula samaki tu wana 34% pungufu ya kutokufa kutokana na matatizo ya moyo ukilinganisha na watu wanaokula nyama mara kwa mara. Huku wanaokula mboga za majani tu wana 20% pungufu  ya kutokufa kutokana na matatizo ya moyo ukilinganisha na watu wanaokula nyama mara kwa mara.

Steve Jobs alizalimwa mwezi Februari 24, mwaka 1955 huko California Marekani na kufariki tarehe 5 mwezi Oktoba mwaka 2011.

Tupe mani yako. Kama kawaida yetu TeknoKona tunakuletea mambo ambayo hukudhani tungeweza kuandika tena kwa lugha penda ya Kiswahili.

Vyanzo: Observer, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kimemeshi kipya cha kuchaji AirPods
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|