Albert Einstein ni moja kati ya wanasayansi ambao mchango wao katika elimu ya fizikia hauta sahaulika, Einstein atakumbukwa kwa formula yake aliyoiandika ya E = mc2 ambayo ni maarufu sana pamoja na mambo mengine mengi katika sayansi.
Leo tunakuletea mambo kadhaa kuhusu mwanasayansi huyu ambayo hayafaahamiki saana kwa watu wengi:-
-
Inasemekana kwamba Albert Einstein alikuwa mzito kuelewa na kujifunza akiwa mtoto.
Inasemekana kwamba Einstein alianza kuongea akiwa na miaka mitatu ama mine kitu ambacho sio cha kawaida kwa watoto, lakini alikuwa na kugeuka mmoja kati ya watu ambao wanadhaniwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
2. Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Albert Einstein (bila ruhusa) alitoa ubongo na baadhi ya sehemu za mwili huo na kisha kuvihifadhi.
Inasemekana daktari huyo alitaka kuchunguza iwapo kama mwanasayansi huyo alikuwa na ubongo wa aina yake kumsaidia kufanya mambo analiyoyafanya, ingawa ukweli ni kwamba daktari huyo hakuwa na utaalamu wa ubongo.
3. Albert Einstein alipewa uraisi wa Israel lakini alikataa ofa hiyo.
Inasemekana kwamba mwanasayansi huyo alikuwa miongoni mwa wanaharakati ambayo walikuwa wanapigania haki za wayahudi. Pengine hii ilimpelekea kupewa ofa hiyo ya kuliongeza taifa la Israeli lakini aliikataa ofa hiyo.
4. Einstein alifeli katika mtihani wa kuingia chuo.
Pengine kutokana na mafanikio yake katika sayansi unaweza kufikiri kwamba Einstein alikuwa na uwezo mkubwa saana lakini kumbukumbu zinaonesha mwanasayansi huyu alifeli alipofanya mtiani wa kuingia chuo na hivyo kuhitaji kusubiri mwaka uliofata.
5. Einstein hakuwa na kumbukumbu nzuri.
Inasemekana kwamba mwanasayansi huyu hakuwa na kumbukumbu nzuri na hasaalikuwa na shida ya kukumbuka majina tarehe ama namba za simu.
Mwanasayansi huyu alifariki dunia mwaka 1955 baada kupata kuvuja kwa damu kwa ndani na alikataaa kufanyiwa upasuaji akisema kwamba anataka kwenda pale wakati wake ukifika na sio kuongeza urefu wa maisha kwa njia mbadala.